WSHIRIKI WA SHINDANO LA KUMSAKA MREMBO WA MKOA WA SHINYANGA 2014 WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WALEMAVU BUHANGIJA NA KUTOA MSAADA WA CHAKULA,HUKU WENGINE WAKISHINDWA KUJIZUIA NA KUTOKWA NA MACHOZI KUTOKANA NA MAZINGIRA MAGUMU WANAYOISHI WATOTO.
Baadhi ya washiriki wa shindano la kumsaka mrembo wa mkoa wa Shinyanga 2014 wakiwa katika kituo cha Buhangija kinacholea watoto wenye ulemavu wa
ngozi,wasioona na wasiosikia ikiwa ni maandalizi yao ya shindano hilo litakalofanyika Juni 28,mwaka huu mjini Kahama na kupambwa na Mzee Yusuph akiwa
amembatana na wasanii wengine kibao watatoa burudani siku hiyo, kabla ya mpambano huo utatanguliwa na shindano la kutafuta mrembo
mwenye kipaji mkoa wa Shinyanga(Miss Talent Shinyanga) kesho Juni
25,2014 katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo mwimbaji wa taarabu
Isha Mashauzi atakuwa akitoa burudani
Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Warembo 20 wanaoshiriki shindano la kutafuta mrembo wa
mkoa wa Shinyanga(Miss Shinyanga 2014) wakiongozwa na mwandaaji wa Mashindano
hayo bi Asela Magaka wa Asela Promotions wametembelea
kituo na kutoa msaada wa vyakula huku wakichangia kidogo walichokuwa
nacho kwenye mifuko yao kuchangia ujenzi wa bweni katika kituo hicho
chenye watoto zaidi ya 260.Pichani ni baadhi ya warembo wakiwa na baadhi
ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wakionesha upendo.
Misaada iliyotolewa na Asela Promotions na kukabidhiwa kwa mkuu wa
kitengo cha Walemavu katika kituo cha Buhangija Jumuishi mwalimu
Bright Mduma ni pamoja na,chumvi katoni 1, mchele kilo 100,unga wa sembe kilo
200,sukari kilo 20,mafuta ya kupikia lita 10,unga wa ngano kilo 50 na sabuni za unga za kufulia kilo
30, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 506,700/=
Watoto wenye ulemavu wakiwa katika eneo la tukio leo.
Aliyesimama
ni mwandaaji wa Mashindano ya Miss Shinyanga mwaka 2014 bi Asela Magaka
kutoka Asela Promotions,ambaye amekuwa akifanya maandalizi ya Mamiss
Tangu mwaka 1999 akizungumza leo katika kituo cha kulelea watoto wenye
ulemavu cha Buhangija mjini Shinyanga.Magaka alisema ameamua kuwapeleka
warembo hao katika kituo hicho ili
kujua mambo yanaoendelea katika jamii ikizingatiwa kuwa kauli mbiu ni
“Urembo,
sanaa na jamii” hivyo ni vyema wakajua kuwa urembo unahusiano na mambo ya jamii,wajue
jamii inahitaji nini,na umuhimu wa kusaidia jamii,hii itasaidia warembo hawa
kuwa mabalozi wazuri katika kusaidia watu mbalimbali wenye mahitaji
maalum katika jamii.
Aliyesimama
ni bwana Mustapha Ramadhani ambaye ni mwalimu wa Mamiss kanda ya ziwa
akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo kufuatia changamoto ya
mabweni aliahidi kuchangia mfuko 1 wa saruji kwa kuungana na Warembo 20
wanaoshiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2014 kuchangia mifuko 18 ya
saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa bweni
la wavulana lililoanza kujengwa 2013 na Miss Tanzania mwaka 2012 Brigette
Alfred.
Kushoto
ni mwandaaji wa shindano la Miss Shinyanga 2014 bi Asela Magaka kutoka
Asela Promotions akikabidhi vyakula(moja ya mifuko ya unga wa sembe)
kwa mkuu wa kitengo cha Walemavu katika kituo cha Buhangija Jumuishi mwalimu Bright Mduma
Baadhi
ya washiriki Miss Shinyanga 2014-Kushoto ni bi Nyangi Warioba kutoka
Msalala kulia ni bi Mary Emmanuel kutoka Ushetu ambao waliguswa na
maisha ya watoto wenye ulemavu na kusababisha watokwe na machozi na
kuamua kuchangia mifuko miwili ya saruji kuchangia ujenzi wa bweni
lililoanza kujengwa na Miss Tanzani mwaka 2012 Brigette
Alfred.Warembo wote 20 wameahidi kuchangia mifuko ya saruji kwa ajili
ya ujenzi huo ikiwa ni kukamilisha mifuko 18 ya saruji.
No comments:
Post a Comment