HAKUNA EBOLA TANZANIA WIZARA YA AFYA YATOA UFAFANUZI
Serikali imethibitisha kutokuwepo kwa ugonjwa wa Ebola hapa nchini.
Kauli hiyo inakuja baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo.
Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dkt.Seif
Rashid ,alisema wagonjwa waliohisiwa kupata maambukizo
kutokana na dalili za awali, ni mmoja kutoka Benin na Mtanzania, lakini
vipimo vimeonesha hawana maambukizo hayo. Amesema tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo. Tayari Mafunzo yametolewa pia kwa wataalamu watakao hudumia wagonjwa iwapo watatokea.
No comments:
Post a Comment