Thursday, August 11, 2016

WANAFUNZI SHULE YA LITTLE TREASURES WAWATEMBELEA WAZEE,ALBINO NA WAGONJWA


Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures iliyopo katika eneo la Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga wametembelea kituo cha walemavu wa ngozi (Albino) cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo mchele,pipi,biskuti,sukari,chumvi,nguo,mafuta ya kujipaka

Wednesday, March 11, 2015

WATU ZAIDI YA 30 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI MBAYA BAADA YA BASI LA ABIRIA KUANGUKIWA NA KONTENA HUKO IRINGA



Tunafuatilia kwa  karibu taarifa ya ajali mbaya sana ambayo imetokea eneo la Changalawe, Mafinga, mkoani Iringa  basi la Majinja toka likitokea Mbeya kwenda Dar es salaam limeangukiwa na kontena na taarifa zisizo rasmi zinasema abiria wengi wamepoteza maisha yao. 

Thursday, December 18, 2014

PROFESA TIBAIJUKA ASEMA KAMWE HAWEZI KUJIUZURU WADHIFA WAKE.

                                                      
Siku Moja baada ya kujiuzuru kwa Mwanasheria mkuu Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.
Profesa Tibaijuka amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa uvumi unaoendelea kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani unawaaminisha wananchi kuwa amehusika katika sakata hilo wakati yeye hajahusika na jambo lolote.
Via :Mwananchi.

ALALA BARABARANI KUCHANGISHA FEDHA KUMSAIDIA MWANAUME ASIYEKUWA NA MAKAO

 

Mwanafunzi anayesoma katika chuo kikuu cha Lancashire nchini Uingereza amekuwa akilala katika barabara za mji wa Preston ili kuchangisha fedha za kumsaidia mwanamume

Wednesday, December 3, 2014

HAYA NDIYO YALIYOJIRI SHINYANGA MKUTANO WA MWIGULU NI BAADA YA KUAPISHA MAKAMANDA

Baadhi ya makamanda wa vijana wa CCM mkoa wa Shinyanga wakila kiapo  baada ya kusimikwa  rasmi kushika wadhifa huo,kutoka kulia ni kamanda wa vijana mkoa Ahmed Salum ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Solwa akifuatiwa  na  Naibu

Thursday, November 27, 2014

MTOTO WA SHULE YA AWALI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI CHENYE FUTI 50


 Kisima chenye urefu wa futi 50 ambapo mtoto Mack  Johnson  amefariki dunia baada ya kutumbukia, Mtoto huyo mwenye umri wa  miaka  (5)alikuwa anasoma darasa la awali katika shule ya Sheer Bliss mtaa wa majengo mapya manispaa  ya Shinyanga.  Ambapo ngazi mbili za jeshi la zimamoto pamoja na kuungwa lakini hazikuweza kufikia kina cha kisima hicho na badala yake ikatumika kamba ndefu na mmoja wa wananchi kujitoa mhanga kutumbukia nayo kisimani kuutoa mwili wa mtoto huyo.

Mashuhuda wamesema tukio hilo limetokea leo  saa tatu  asubuhi ambapo mtoto huyo alitumbukia kwenye kisima hicho wakati akicheza na wenzake karibu na kisima hicho kilichopo eneo la shule ambacho kimefunikwa na makaravati yaliyoonekana kuchakaa.
Mwili wa mtoto Mack Johnson ukitolewa kwenye kisima cha maji na wananchi waliofika eneo la tukio wakishirikiana na jeshi la wananchi na jeshi la zimamoto na uokoaji.

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa eneo la tukio Dkt  Anselm Tarimo amesema  wamebaini kuwa mazingira ya shule hiyo siyo rafiki, shimo lilikuwa halijafunikwa hivyo kuwaomba wataalam mbalimbali wawe wanapita katika maeneo wanakosomea watoto ili kujua mazingira ya watoto kuepusha majanga yanayoepukika.
 

BARIDI YAGANDISHA BREKI ZA NDEGE ABIRIA WALAZIMIKA KUSHUKA NA KUISUKUMA


Abiria waliokuwa wanafanya safari na shirika ka ndege la Serbia walilazimika kushuka katika ndege hiyo na kuisukuma baada ya breki zake kuganda na kushindwa kuondoka.