Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures iliyopo katika eneo la Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga wametembelea kituo cha walemavu wa ngozi (Albino) cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo mchele,pipi,biskuti,sukari,chumvi,nguo,mafuta ya kujipaka, sabuni,miswaki na dawa ya meno ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa shule hiyo Julai mwaka 2011.
Wanafunzi hao mbali na kutembelea kituo cha Buhangija,pia wametembelea katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na kituo cha kulelea wazee wasiojiweza cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga na kuwapatia msaada kama waliotoa katika kituo cha Buhangija.
Shule ya Little Treasures yenye wanafunzi zaidi ya 500 imejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia kwa watoto hali inayosababisha watoto kupata elimu bora inayoendana na sayansi na teknolojia.
Wanafunzi wakiwasili Buhangija : Shule ya Little Tresures inafundisha masomo ya Kiingereza,Kifaransa,Kiswahili na ujasiliamali ikiwemo ufugaji wa samaki,ng'ombe wa kisasa.
Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Little Treasures Samburu Caleb akizungumza katika Kituo cha Buhangija ambapo alisema shule hiyo imeamua kuadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake Julai mwaka 2011 kwa kutembelea kituo hicho, kambi ya wazee Kolandoto na kutembelea wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Mwalimu Caleb alivitaja vitu vilivyotolewa na wanafunzi wao katika vituo vyote vitatu kuwa ni mchele, sukari,chumvi,nguo,mafuta ya kujipaka, sabuni,miswaki na dawa ya meno vyote vikiwa na thamani ya shilingi 750,000/=
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiwa katika kituo cha Buhangija
Watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasiosikia na wasioona wakiwa katika kituo cha Buhangija
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakitoa burudani ya wimbo katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiimba
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kituoni
Mmoja wa walezi wa watoto kwenye kituo cha Buhangija Flora Kankutebe akiwa na watoto
Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Little Treasures Samburu Caleb akimpa mwanafunzi wake mfuko wenye sabuni,mafuta ya kujipaka,chumvi na vitu vingine vingi ili akabidhi kwa watoto wa kituo cha Buhangija
Mwanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures akitoa zawadi kwa mtoto mwenye albinism
Mwanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures akiendelea kugawa zawadi
Magari ya wanafunzi hao
Wanafunzi wakiwa ndani ya gari
Agosti 10,2016-Hapa ni katika kituo cha wazee wasiojiweza cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga.Hawa ni baadhi ya wazee katika kituo hicho wakiwa wamekaa baada ya wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures kuwasili katika kituo hicho
Msimamizi wa kituo cha wazee cha Kolandoto Sophia Kang'ombe akiwakaribisha wanafunzi hao,ambapo alisema kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 1917 sasa kina jumla ya wazee 14 na watoto 8
Mwenyekiti wa kituo cha Kolandoto,mzee Samora Maganga akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures
Wazee wanaoishi katika kituo cha Kolandoto
No comments:
Post a Comment