JESHI la Polisi mkoani Simiyu linamshikilia kada wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Ramadhani Busega ambaye ni Mwenyekiti wa Kata ya
Mawamanyili
, wilayani Busega kwa tuhuma za ujambazi na ubakaji.
Pia linaendelea kumsaka Mchumi wa CCM Wilaya ya Busega, Mashaka Obedi
ambaye anadaiwa kukimbia baada ya kufanya uporaji wa sh milioni 20
katika nyumba ya Mwalimu Samwel Mkumbo anayeishi kitongoji cha Nassa
Ginnery, Kijiji cha Mwagulanja wilayani humo.
Baada ya kupora inadaiwa
walivamia chumba cha mwalimu mwingine ambaye alikuwa amepanga kwenye
nyumba hiyo na kumbaka.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo, Msoka
na wenzake walidaiwa kufanya tukio hilo saa 7 usiku kuamkia Agosti 28
mwaka huu, kijijini humo na kisha kutoweka, ambako Jeshi la Polisi
limewatia nguvuni
baadhi na kuendelea kumsaka mchumi huyo wa CCM.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa njia ya simu, Kamanda Mkumbo,
alisema ni kweli tukio hilo limetokea na watu wengine kadhaa
wanashikiliwa.
Kamanda Mkumbo, aliwataja wengine wanaoshikiliwa ni Libent Rwegarulila
ambaye ni Mshauri wa Mahakama ya Mwanzo ya Nyashimo wilayani Busega,
Mkurugenzi wa NGO’s moja inayojishughulisha na masuala ya wazee wilayani
Magu, Nkondo Kubini na Meshack Samson ambaye ni mfanyabiashara wa duka
la rejareja kijijini hapo, wote wakiwa wakazi wa Nassa Ginnery.
Alisema kwamba, watuhumiwa hao walipomvamia mwalimu huyo walimpora sh
milioni 20 kabla ya kuingia katika chumba cha mpangaji wake ambaye pia
ni mwalimu na kumbaka kwa zamu.
Hata hivyo, alisema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba
hatosita kumfikisha mtu katika vyombo vya sheria kutokana na kosa
walilofanya, hata kama wametoka katika chama tawala kwa kuwa viongozi
wanatakiwa kuwa mfano na si kufanya mambo mabaya katika jamii.
Chanzo :Tanzania daima
No comments:
Post a Comment