Baadhi ya washiriki wa semina ya elimu ya hifadhi ya jamii iliyoandaliwa na mamlaka ya usimamizi wa sekta ya mifuko hiyo SSRA kutoka makao makuu jijini Dar es salaam wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
Mwezeshaji wa semina hiyo kutoka SSRA Salma Maghimbi akifafanua jinsi mamlaka hiyo inavyofanya kazi na mifuko ya hifadhi ya jamii katika kuhakikisha wanachama wake wananufaika kupitia pensheni watakazolipwa baada ya kustaafu ama kupata majanga.
Katibu wa chama cha walimu mkoa wa Shinyanga (CWT)Rehema Sitta akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi baada ya hotuba nzuri aliyoitoa iliyolenga zaidi kuboresha mishahara ya wafanyakazi,kurekebisha kasoro zilizopo katika malipo ya pensheni kwa wastaafu na kutoa tahadhari kwa walimu na wafanyakazi wote kuwa makini wakati wa uchaguzi wasitumiwe kupata viongozi wasio na sifa. |
No comments:
Post a Comment