Saturday, May 17, 2014

UKAWA WATIKISA MJI WA SHINYANGA ,MAELFU YA WANANCHI WAFULIKA UWANJANI.JIONEE ILIVYOKUWA.

Mbunge wa jimbo la Maswa mashariki Sylvester Kasulumbayi akizungumza na maelfu ya wananchi wa manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA),ambapo aliwataka kuhakikisha wanatunza vitambulisho vyao vya kupiga kura na ambao wametimiza miaka 18 wajiandikishe ili watimize haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi wanayemtaka atakaye waletea maendeleo.

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Shinyanga wakishangilia baada ya mbunge wa Maswa mashariki Kasulumbayi kupanda jukwaani na kutoa nasaha kwa wananchi.

Kiongozi wa msafara wa UKAWA katika mikoa ya kanda ya ziwa Masena Nyambabe akiwataka wananchi kuwa makini na mchakato wa katiba mpya,ili kuhakikisha inapatikana katiba iliyobora itakayotokana na maoni ya wananchi na si vinginevyo huku akisisitiza kuwa kamwe UKAWA hawatarudi nyuma katika kupigania haki za watanzania.

Mwenyekiti wa baraza la vijana wa CHADEMA taifa(BAVICHA) John Heche,akiwa katika mkutano wa hadhara wa UKAWA uwanja wa Shycom manispaa ya Shinyanga,ambapo alisema CCM ikianguka watu wengi wataumia kwa kuwa ni mafisadi na kuwataka watanzania kuunga mkono UKAWA ili waweze kuing'oa  madarakani. Alisema rasmu ya katiba iliyotolewa na tume ya mabadiliko ya katiba inastahili kupongezwa kwa kuwa ilifanya kazi kubwa ya kukusanya maoni ya watanzania na kuyafikisha bila kuficha likiwemo suala la serikali tatu ambazo wanaziunga mkono.

No comments:

Post a Comment