MASHINDANO ya kumsaka
miss Shinyanga Centre yanatarajiwa kufanyika mei 23 mwaka huu katika ukumbi wa NSSF manispaa ya Shinyanga, huku warembo 10
watapanda jukwaani kugombea taji hilo kwa mwaka 2014.
Licha ya mashindano hayo maandalizi yake kukamilika lakini yanakabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo idadi ya washiriki kuwa ndogo,kutokana na
baadhi ya wazazi kuwazuia watoto wao kushiriki kwa madai kuwa ni uhuni hivyo
kupelekea idadi ya washiriki kuishia 10 na kushindwa kuleta changamoto kubwa.
Muuandaaji wa mashindano hayo Elizabeth Stephen,anawaomba wazazi
pindi mashindano kama hayo yakitokea wawaruhusu
mabinti zao kushiriki zoezi la kumsaka miss shinyanga
centre, kwani umiss ni fani na ni kipaji kama ilivyo kwa vipaji vingine vya
wachezaji wa mpira wa miguu na pete.
“ mpaka sasa kuna warembo kumi tu ambao wanashiriki
kinyanyanyiro hicho, hivyo ni vema wazazi wakawaruhusu mabinti zao ili kuleta
changamoto kwa washiriki, badala ya ilivyo sasa idadi ni ndogo haina changamoto
kubwa”alisema muandaaji huyo Elizabeth.
Baadhi ya washiriki wa miss shinyanga centre Grace Kimaro
Yunice Kidaha walisema hakuna uhuni ndani ya zoezi la umiss bali
uhuuni ni tabia ya mtu, hivyo wazazi wawaruhusu watoto wao ili waweze kusrikiki
mashindano.
Hata hivyo washiriki
wote kwa nyakati tofauti kila mmoja alijigamba kutwaa taji hilo kwa kuwamwaga wengine,ambapo
walibainisha kuwa mshindi atakaye ibuka kutwaa taji hilo atatoa kipaumbele kwa
jamii kuielimisha kuachana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBONO )
na vikongwe.
No comments:
Post a Comment