Sunday, August 3, 2014

HAYA NDIYO YALIYOJIRI JIMBO LA SOLWA JIONEE PICHA NA TUKIO ZIMA.

Ngoma ya waswezi ikiburudisha katika mkutano wa hadhara uliofanyika  kijiji cha Igalamya kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum ambaye aliuatana na mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hamad  pamoja na  viongozi wengine wa serikali.

Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum  kujibu maswali aliyoulizwa na wananchi wa kata ya Usule juu ya huduma za afya ikiwemo kutozwa fedha pindi wanapohitaji msaada wa gari la wagonjwa.

Gari la kubeba wagonjwa ambalo lilitolewa na wa jimbo la Solwa Ahmed Salum  kwaajili ya  kuwabeba wagonjwa walio mahututi,wajawazito na wale watakao pata ajali bure,lakini wananchi wamekuwa wakilalamika kutozwa fedha na watumishi wa idara ya afya kwenye zahanati na vituo vya afya kiasi cha sh 40,000 mpaka 60,000 kwa ajili ya kununua mafuta   huku akisisitiza kuwa huduma hiyo itatolewa bure na mafuta yatakuwepo ya kutosha wakati wote.

Gari hii iliharibika hapo awali na kukaa muda mrefu bila matengenezo kisha  mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum aliamua kutengeneza kwa kiasi cha  7.5 miion na kuwakabihi wananchi wa kata ya Usule  huku akiwapa angalizo juu ya utumiaji wa gari hiyo ambalo ni kwa ajili ya wagonjwa mahututi,wanawake walioshindwa kujifungua wanahitaji msaada wa kupelekwa hospitai ya rufaa ya mkoa na waliopata ajali na hakuna malipo yoyote huduma ni bure.


Mbunge Azzah Hilali alisimama na kuongelea kukerwa na baadhi ya wanaume kuwapatia mimba wasichana wa shule huku wazazi au walezi wa pande mbili kukutana na kumalizana kinyemela  hilo limekuwa ni tatizo hivyo kuna sheria inayoundwa mwanafunzi akipata mimba wazazi wote wa pande mbili wanashitakiwa mahakamani kwani  wanapofanya hivyo wanamnyima mtoto wa kike haki yake ya kupata elimu bora na kuendeleza wimbi la umasikini kwani hata wewe mzazi ukipewa ng'ombe tano hazina thamani kama elimu atakayo ipata mtoto wa kike  katika maisha yake.


Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mohamed Kiyungi akimpatia vielelezo mbunge wa jimbo hilo kutokana na changamoto zilizoulizwa  ili kuweza kuzipatia majibu katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment