Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Chenge Mwl. Steven Masinde iliyopo wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu akionyesha shimo lililochimbwa kwa ajili ya kutafuta maji.
Walimu
Shule ya sekondari Chenge iliyopo katika Halmshauri Mji wa Bariadi mkoani
Simiyu wanakabiliwa na na changamoto mkubwa ya uhaba wa maji hali inayowafanya
wao pamoja na wanafunzi kushindwa kuhimili hali hiyo na kuamua kuondoka shuleni
hapo kila siku kabla ya muda.
Walisema
hali hiyo imeongeza utoro kwa wanafunzi na wakati mwingine kusababisha baadhi
ya masomo kutofundishwa kutokana na wanafunzi kutumia muda huo, kufuata maji
umbali wa kilometa moja katika mto wa nyaumata ambao walisema nao umekauka.
Akiongea
na wandishi wa habari shuleni hapo kaimu mkuu wa shule hiyo Steven Masinde
alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo kwa muda wa miaka 7 wamekuwa
wakiangaikia kero hiyo kuipeleka katika ngazi za juu za serikali lakini bila ya
mafanikio.
Masinde
alibainisha kuwa mwaka 2010 wananchi wa kijiji walichimba kisima shuleni
hapo, na kuishia katikati bila ya kumalizika. Huku diwani wa kata Robert
Rweyo naye akichimba shimo ambalo nalo lilishia njiani bila ya kumalizika.
“kwa
sasa shule imejaa mashimo..ambayo ni hatari kwa wanafunzi hata familia za
walimu wanaoishi katiba nyumba za shule..kuna shimo la wananchi halikumalizika,
lakini diwani naye alichimba akakomea njiani..yote yapo hayana kazi na sasa
yameanza kutupiwa uchafu na wanafunzi” Alisema Masunga.
Alisema
kuwa walimu wengi wanaoletwa shuleni hapo wamekuwa wakikataa kuishi karibu na
shule hiyo kutokana na kukosa maji hata ya kunawa mara baada ya kutoka darasani
kwa ajili ya kutioa uchafu wa chaki, huku wanafunzi wakikosa hata maji ya
kunywa.
Aidha
alisema kuwa walimu wengi wamekuwa wakiishi mjini Bariadi ambapo ni urefu wa
kilometa 10 kutoka shuleni hadi mjini, jambo linalosababisha walimu hao
kuondoka shuleni hapo kabla ya muda wa kazi.
Hata
hivyo Masinde alisema wameanziasha mpango wa chakula kwa wanafunzi hususani
madarasa yenye mitihani, kidato cha pili na nne lakini wanashindwa kumudu kwa
sababu ya kukosa maji na kuwalazimu wanafunzi waache vipindi na kwenda kutafuta
maji katika mto nyaumata.
Alibanisha
maji ya mto huyo yamekuwa siyo salama na kutishia uhai wa maisha yao, kutokana
mto huo kukauka hali inayowalazimu kuchimba mashimo kwa ajili ya kupata maji,
huku wakichangia mto huo pamoja na mifugo.
Hata
hivyo shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 232 ilianzishwa mwaka 2007
inakabiliwa na uhaba wa walimu wa sayansi hadi sasa ina mwalimu mmoja wa
sayansi ikiwa pamoja na ukosefu wa nyumba za walimu na thamani za ofisi.
No comments:
Post a Comment