Mbali na mauaji ya albino na vikongwe ambayo
yalipata kutikisa katika maeneo kadhaa ya nchi, wauaji wa kukodi
wanatumika kutekeleza uhalifu huo kwa lengo la kulipiza kisasi, uporaji
wa fedha, kujitanua kibiashara au kudhulumu mali na fedha.
Uchunguzi wa muda mrefu uliofanywa na gazeti hili
umebaini kuwa silaha nyingi zinazotumika katika mauaji ya kukodi
yanayofanyika mikoa ya Kanda ya Kaskazini, hununuliwa ama kukodishwa
kutoka Namanga upande wa Kenya.
Wauzaji wa silaha hizo ni ama raia wa Kenya wenye
asili ya Kisomali ama wahamiaji haramu wenye asili ya Kisomali
wanaoingia nchini, wakitokea Somalia kupitia Kenya.
Uchunguzi umebaini kuwa bunduki aina ya Submachine
Gun (SMG) huuzwa kati ya Sh3 milioni hadi Sh5 milioni na bastola
zikiuzwa kati ya Sh500,000 na Sh1.2 milioni.
Pamoja na kutoka nje ya nchi, wauaji wengine wa
kukodi hupatikana nchini kulingana na aina ya mtu wa kuuawa, mazingira
na ugumu wa kazi.
Kwa Tanzania, mikoa inayoongoza kwa kuwa na wauaji
wa kukodi ni Arusha na Manyara na Mkoa wa Kilimanjaro umekuwa ukiguswa
kuwa jirani na mikoa hiyo.
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mtoa
taarifa wetu alisema alisema: “Hata sasa ukihitaji vijana wa kazi
nitakuunganisha. Jambo muhimu hakikisha huwarushi (unawapa fedha zao),
ukiwarusha lazima na wewe watakuua.”
“Yupo rafiki yangu anayewafahamu vyema kwa sababu
amewahi kuwaunganisha na waliokuwa wakihitaji huduma yao,” alisema mtoa
habari huyo.
Malipo ya kuua
“Malipo kwa kazi hii yanaanzia kati ya Sh1 milioni
na Sh5 milioni kutegemea na uzito wa kazi husika,” alisema mtoa taarifa
wetu anayeishi Arusha na akithibitisha kwamba anafahamiana na madalali
wa wauaji hao.
Alisema mara nyingi wauaji hao hawataki kukutana
na wateja moja kwa moja ili kuepuka kutambulika, badala yake hukutana au
kuwasiliana na mtu wa kati (wakala) ambaye pia hupokea malipo na
kuwakabidhi
VIA: Mwananchi.
VIA: Mwananchi.
No comments:
Post a Comment