|
Mwanasheria mwandamizi wa mamlaka ya usimamizi wa sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii (SSRA) Salma Maghimbi kutoka makao makuu jijini Dar es salaam,akizungumza na watumishi kutoka jeshi la pilisi mkoa wa Shinyanga kwenye ukumbi wa Ibanza hotel manispaa ya Shinyanga.
Mwanasheria huyo aliwataka askari na watumishi wengine kuhakikisha wanafanya utafiti wa kina kabla ya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwani kwa sasa sheria imefanyiwa marekebisho hivyo wanaruhusiwa kuchagua mfuko wanaoutaka. |
|
Watumishi wa jeshi la polisi mkoa wa shinyanga wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na mwanasheria mwandamizi juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na haki zao katika mifuko hiyo. |
|
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya akifungua semina ya siku moja kwa watumishi wa jeshi hilo iliyoandaliwa na SSRA,ikilenga kutoa elimu juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na kuitambulisha mamlaka hiyo ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa mifuko ya hifadhi ya jamii. |
|
Afisa mfawidhi wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga,akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa semina ya mifuko ya hifadhi ya jamii juu ya mikopo kwa wanachama,ambapo alisema mikopo inayotolewa ni ya nyumba kwa watumishi hatua hiyo inatokana na kuona hitaji kubwa ni kupata nyumba kupitia mafao yao. |
|
Pc -Rose kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga akitakakupatiwa ufafanuzi na wawezeshaji wa semina hiyo,je ni kwa nini jeshi la polisi lisiwe na mfuko mmoja tu wa hifadhi ya jamii badala ya kutumia mifuko mbalimbali. |
|
Meneja wa
mkoa mfuko wa taifa wa bima ya afya Immanuel Amani akiwataka watumishi hao kutumia huduma za bima ili kurahisisha gharama za matibabu ambazo kwa sasa zinazidi kupanda . |
No comments:
Post a Comment