Tuesday, September 2, 2014

MREMBO ALIYETAKIWA KUREJESHA TAJI LAKE AGOMA

Mya Myat anataka aombwe msamaha na waandalizi wa shindano la taji hilo
Mshindi wa taji la urembo nchini Burma aliyenyang'anywa taji lake wiki iliopita ,amekataa kurudisha taji hilo kwa waandalizi wa mashindano hayo Korea Kusini.
Katika kikao na wanahabari,Mya Myat Noe amesema kwamba atarudisha tu taji hilo lenye thamani ya dola 100,000, ikiwa ataombwa msamaha na waandalizi wa mashindano hayo.
Bi May alishinda mashindano ya Miss Asia Pacific World mwaka 2014 iliyofanyika mwezi Mei mjini Seoul.
Wiki jana waandalizi walimshtumu kwa kukosa shukrani na kutokuwa mkweli.
Bi May ni mshindi wa kwanza wa shindano hilo nchini Burma , kulingana mwandishi wa BBC Jonah Fisher.
Waandalizi wanasema mshindi huyo aliwadaganya na kuwadharau madai aliyoyakanusha
Mrembo huyo alidaiwa kutoroka na taji hilo, madai ambayo ameyakanusha.
Bi May aliwaambia wanahabari kuwa alilazimishwa kudanganya kuhusu umri wake na waandalizi hao pia walimshurutisha kuwekwa matiti bandia.
Hata hivyo amekana madai ya kuwa alitoroka na taji hilo akisema kuwa aliabiri ndege kuelekea Myanmar bila kufahamu kuwa alikuwa ashavuliwa taji hilo.
Waandalizi walidai kuwa mwanadada huyo aliwadanganya na kuwadharau, ila hawakutoa maeleo zaidi.
Baadaye ilifahamika kwamba kulikuwa na mtafaruku kati ya mamake May na waandilizi hao kuhusiana na vipi Bi May anaweza kusimamiwa .

No comments:

Post a Comment