Thursday, November 27, 2014

MTOTO WA SHULE YA AWALI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI CHENYE FUTI 50


 Kisima chenye urefu wa futi 50 ambapo mtoto Mack  Johnson  amefariki dunia baada ya kutumbukia, Mtoto huyo mwenye umri wa  miaka  (5)alikuwa anasoma darasa la awali katika shule ya Sheer Bliss mtaa wa majengo mapya manispaa  ya Shinyanga.  Ambapo ngazi mbili za jeshi la zimamoto pamoja na kuungwa lakini hazikuweza kufikia kina cha kisima hicho na badala yake ikatumika kamba ndefu na mmoja wa wananchi kujitoa mhanga kutumbukia nayo kisimani kuutoa mwili wa mtoto huyo.

Mashuhuda wamesema tukio hilo limetokea leo  saa tatu  asubuhi ambapo mtoto huyo alitumbukia kwenye kisima hicho wakati akicheza na wenzake karibu na kisima hicho kilichopo eneo la shule ambacho kimefunikwa na makaravati yaliyoonekana kuchakaa.
Mwili wa mtoto Mack Johnson ukitolewa kwenye kisima cha maji na wananchi waliofika eneo la tukio wakishirikiana na jeshi la wananchi na jeshi la zimamoto na uokoaji.

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa eneo la tukio Dkt  Anselm Tarimo amesema  wamebaini kuwa mazingira ya shule hiyo siyo rafiki, shimo lilikuwa halijafunikwa hivyo kuwaomba wataalam mbalimbali wawe wanapita katika maeneo wanakosomea watoto ili kujua mazingira ya watoto kuepusha majanga yanayoepukika.
 

No comments:

Post a Comment