Wednesday, July 9, 2014

MAKUBWA YAIBUKA MAFUNZO YA UZAZI WA MPANGO KANDA YA ZIWA NA MAGHARIBI

Waandishi wa habari kutoka kanda ya ziwa na Magharibi wamepatiwa mafunzo ya uzazi wa mpango ili kwenda kutoa elimu kwa jamii umuhimu wa kutumia uzazi wa mpango kupitia taaluma yao, kutokana na mikoa iliyopo kanda hizo bado iko nyuma kutumia uzazi wa mpango hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka vifo vya wakinamama na watoto wachanga.        Mikoa hiyo ni Kigoma,Mwanza,Shinyanga,Tabora,Mara na Kagera ambapo mkoa wa mara ni wa mwisho kwa matumizi ya uzazi wa mpango ambapo  wanaotumia ni asilimia 10,ukifuatiwa na mkoa wa Mwanza asiimia 12,Shinyanga 13 na Kigoma asilimia 14.
Wataalamu wa uzazi wa mpango ambao pia ni wawezeshaji wa mafunzo ya uzazi wa mpango kwa waandishi wa habari wa mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi.
Afisa uzazi wa mpango kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii ,kitengo cha afya ya uzazi na mtoto Zuhura  Mbuguni,akiwataka waandishi wa habari kusaidia kuihamasisha jamii kutumia uzazi wa mpango na kuachana na imani potofu ambazo haziwezi kuwasaidia kuzuia mimba na kupata idadi ya watoto wanaowataka.    Alisema baadhi ya watu katika jamii bado wanaimani potofu za kutumia njia ambazo siyo sahihi mfano kuloweka majivu na kunywa wakiamini zinaweza kuwasaidia jambo linahitaji elimu zaidi kutolewa pamoja na baadhi ya wanaume kuwazuia wake zao kutumia uzazi wa mpango na ndugu katika ukoo kuwatenga wanawake kwa kuchelewa kuzaa mtoto mwingine baada ya kutumia njia hiyo na kupelekea kuvunja mji.

Mwandishi wa habari wa ITV kutoka mkoa wa Simiyu Berensi China ,akizungumza kwenye mafunzo hayo ambapo alisema bado kuna changamoto kubwa kuielimisha jamii ione umuhimu wa kutumia uzazi wa mpango na aliitaka wizara kuwawezesha waandishi wa habari kwenda vijijini kufanya uchunguzi na kuihamasisha jamii kupitia vyombo vya habari.
Waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo
Washiriki wa mafunzo ya uzazi wa mpango wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupatiwa elimu na wataalamu wa afya.
Mafunzo yanaendelea
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Anna Mwalongo alisema changamoto iliyopo ni
wasichana kubeba mimba chini ya miaka 20 ni tatizo kubwa kwani  anaweza kupoteza maisha yeye na mtoto  kutokana na viungo vyake vya mwili havijakomaaikilinganishwa na wanaozaa wakiwa na umri unaotakiwa. pia kuzaa katika umri mkubwa kuanzia  miaka 35 ni hatari mwanamke anatakiwa awe chini ya uangalizi wa daktari pia alisema uzazi salama kwa wanawake ni mimba ya kwanza hadi ya nne zaidi ya hapo anapaswa kumueleza mtaalamu ili ampe ushauri wa kitaalamu.
Washiriki wa mafunzo ya uzazi wa mpango wakiwa katika picha ya pamoja na mgaga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Ntuli Kapologwe
Mafunzo yanaendelea
Washiriki wa mafunzo

Mwandishi wa habari wa kampuni ya mwananchi Communications Jackline Masinde kutoka mkoa wa Geita akichangia kwenye mafunzo hayo katika kuhakikisha changamoto zinazochangia jamii kushindwa kutumia uzazi wa mpango na njisi ya kukabiliana nazo.
Washiriki wa mafunzo ya uzazi wa mpango wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupatiwa elimu na wataalamu wa afya.












No comments:

Post a Comment