|
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Mwanvua Jilumbi akifungua warsha ya
wadau wa ngozi Mkoani Simiyu, iliyokuwa na lengo la kujadili mfumo mpya
wa kukusanya ushuru unatokana na zao la ngozi. akifungua warsha hiyo
katibu tawala huyo alieleza kuwa mkoa wa simiyu kwa mwaka 2013/14 hakuna
hata senti moja ilikusanywa kutokana na ushuru wa ngozi, licha ya mkoa
huo kuwa na idadi kubwa ya mifugo kama ngo'mbe, mbuzi, pamoja na
kondoo. alisema kuwa idadi kubwa ya wafugaji wamekuwa hawatozwi ushuru
pindi wanapoleta ngozi zao kuwauzia wafanyabishara wanaosafirisha zao
hilo nje ya nchi. sambammba na hayo Jilumbi alieleza kuwa Mkoa wa Simiyu
una idadi ya ng'ombe wapatoa Milioni 1.5 idadi aliyosema kuwa
inalingana na watu walioko mkoani hapa.
alisema kuwepo kwa magendo ya bishara ya zao hilo imekuwa changamoto
kubwa inayosababisha serikali kukosa ushuru unaotokana na ngozi, ambapo
aliwataka washiriki wa warsha hiyo kujadili kwa kina jinsi ya serikali
inatakavyokusanya ushuru unaotokana na zao hilo.
|
|
|
|
|
Washiriki wa warsha hiyo wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa simiyu Mwanvua Jilumbi wakati akifungua warsha.
|
Picha na Simiyu news Blog
No comments:
Post a Comment