Mkulima kutoka mkoani Mara bwana Godfrey Mukiri ambaye alisisitiza wakulima waliopata hasara baada ya kulima mbegu za pamba UK91 walipwe fidia huku akiomba kuanzishwa viwanda vya nyuzi na nguo hapa nchini badala ya kutegemea viwanda vya nje vinavyosababisha bei ya pamba kushuka kila kukicha. Changamoto zilizotajwa kuzorotesha zao la pamba ni pamoja na uchafuzi wa pamba,uuzaji wa pamba ghafi nje ya nchi,pembejeo,kilimo cha kutegemea mvua,mabadiliko ya tabia nchi,udanganyifu(wizi) katika mizani na wakulima wa pembezoni kutokuwa na taarifa za kutosha kuhusu zao la pamba. |
Aliyesimama ni katibu tawala mkoa wa Shinyanga Anselm Tarimo akizungumza katika kongamano hilo ambapo pamoja na mambo mengine mbali na kupigia debe kilimo cha pamba pia alisisitiza wananchi kulima mtama,alizeti na ufuta |
Wadau mbalimbali wakiwemo wakulima,wakuu wa wilaya,makatibu tawala,waandishi wa habari,wafanyakazi wa MVIWATA kutoka makao makuu wamehudhuria kongamano hilo |
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga aliyekuwa mgeni rasmi kwa
niaba ya wakuu wa mikoa minne inayolima zao la pamba kanda ya ziwa
akifungua mkutano huo wa wadau wa zao la pamba ambapo alisema unalenga
kubadilishana mawazo kuhusu mbegu za UK91 zinazozalishwa na kusambazwa
na kampuni ya Quoton ambazo baada ya kupandwa katika baadhi ya maeneo
hazikuota na kuwatia hasara wakulima wa zao la pamba.
Kaimu mkurugenzi wa bodi ya pamba bwana
Gabriel Mwalo akizungumza katika kongamano hilo ambapo alisema njia ya
kutatua changamoto katika zao la pamba ni kilimo cha mkataba huku
akiwashauri wakulima kujiunga katika vikundi na kupitia vikundi hivyo
wanakikundi wataweza kununua pamba kutoka kwa wanachama na wanunuzi wa
pamba watanunua pamba kutoka kwenye vikundi ili kuepukana na mawakala
wasio waaminifu wanaonyonya wakulima
Aliyesimama ni bwana Joseph Ngura
kutoka taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania(TOSCI) akizungumza
katika kongamano hilo ambapo alisema miongoni mwa changamoto
wanazokabiliana nazo ni pamoja na wakulima kutozingatia sheria za mbegu
kwani wengine wanachanganya pamba na mazao mengine
|
No comments:
Post a Comment