Mimba za utotoni ni chanzo kikubwa cha kuongezeka kwa vifo vya watoto wachanga kanda ya ziwa na Magharibi inayohusisha mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Kigoma,Tabora ,Kagera ,Simiyu,Geita na Mara taarifa ambayo ilitolewa na mtaalamu wa uzazi wa mpango kutoka mkoa wa Shinyanga Anna Mwalongo.
Alisema watoto wanaozaliwa na watoto wenzao wanakufa mapema kutokana na uangalizi kutokuwa mzuri ukilinganisha na mtoto aliyezaliwa na mama aliyefikisha umri unaotakiwa kuanzia miaka 20.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya uzazi wa mpango yaliyoanza juzi mjini Shinyanga ambayo yamemalizika leo. |
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo aliyokuwa akitoa mratibu wa uzazi wa mpango kanda ya ziwa. |
Uwasilishaji wa kazi za vikundi ambazo zililenga kuainisha mtazamo potofu uliopo kwenye jamii juu ya matumizi ya uzazi wa mpango. |
Waandishi wa habari kutoka mkoa wa Geita na Kigoma |
Mjumbe kutoka mkoa wa Tabora akiwasilisha masuala mbalimbali waliyoyabaini juu ya uvumi na imani potofu kutumia uzazi wa mpango. |
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uzazi wa mpango wakiwa katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga. |
Waandishi wa habari kutoka mkoa wa Tabora wakiwa katika majadiliano ya namna ya kuondoa changamoto zilizopo ambazozinasababisha wanawake kushindwa kutumia uzazi wa mpango. |
No comments:
Post a Comment