Monday, November 3, 2014

BREAKING NEWS: MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE BUSEGA AFARIKI DUNIA SAA CHACHE KABLA YA KUINGIA CHUMBA CHA MTIHANI.



Habari tulizozipata hivi punde kutoka mkoani Simiyu ni kwamba mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Yunis Festo aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika shule ya sekondari Simba wa Yuda iliyoko katika kijiji cha Bulima wilaya ya Busega amefariki dunia .

Mwanafunzu huyo amefariki dunia  saa 11 alfajiri ya leo zikiwa zimesalia saa chache kuanza kufanyika kwa mtihani wa kidato cha Nne kote nchini ulioanza leo.

Mdau wa Malunde1 blog bwana Damian Kageba Lupimo aliyeko eneo la tukio anasema mwanafunzi huyo amefariki dunia alfajiri ya leo saa 11 baada ya kukimbizwa  katika kituo cha afya  Bulima na wanafunzi wenzake aliokuwa nao bwenini alipozidiwa majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo.

Habari zinasema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa anaumwa kichwa na kwamba alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Sickle Cell.

Damian Kageba Lupimo anasema pamoja na wanafunzi wengine wa kidato cha nne kuendelea na mitihani yao kama kawaida lakini hali ya majonzi imetawala katika shule hiyo.
Via Malunde Blog.

No comments:

Post a Comment