|
Askofu Emanual Makala wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya kusini mashariki ya ziwa victoria akiweka jiwe la msingi katika jengo la bweni la wavuana shule ya sekondari Mwadui wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga. Akiwa shuleni hapo askofu Makala alisisitiza suala la maadili kwa wanafunzi na kutoa wito kwa wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuimarisha maadili kwa watoto huku akisisitiza kuwa hawatakuwa na huruma wala msamaha kwa mwanafunzi atakaye kiuka sheria za shule ikiwemo kuvaa sketi fupi,suruali mlegezo na kukutwa na simu.
Askofu makala alisema wakishirikana ipasavyo
, pamoja na kufuatilia taarifa za watoto wao shuleni itasaidia kwa kiwango
kikubwa kuongeza taaluma ya wanafunzi na kupata ufaulu mzuri sanjari na
kuzalisha taifa la wataalamu na viongozi wenye maadili.
Askofu Makala pia alifungua na kuweka jiwe
la msingi katika bweni Jipya la wavulana ambalo limegharimu Sh 39 milioni
zikiwa ni fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo,wadhamini,wanafunzi pamoja na
washirika wa kanisa hilo huku idadi ya wanafunzi ikiwani ni 282 kati yao
wasichana ni 148 na 134 wavulana.
| |
|
|
Askofu Emmanuel Makala akiwa katika jengo la bweni la wavulana mara baada ya kuweka jiwe la msingi pembeni yake ni mchungaji Yohana Nzelu ambaye pia ni mkuu wa shule ya sekondari Mwadui.
|
|
Ufunguzi umekamilika |
|
Mchungaji Yohana Nzelu na viongozi wengine wakielekea eneo lilipojengwa bweni la wavulana. |
Hata hivyo uongozi wa shule ya sekondari Mwadui iliyopo
ndani ya Mgodi wa madini ya Almasi( Wiliamson Diamond) wilayani Kishapu mkoa wa
Shinyanga,umetoa onyo kali kwa baadhi ya wanafunzi wasiozingatia maadili kwa
kuvaa suruali mlegezo,sketi fupi,kuwa na simu pamoja na kutumia vipodozi.
Onyo hilo lilitolewa na mkuu wa shule hiyo
Mchungaji Yohana Nzelu kwenye kikao cha bodi ya shule na wazazi ,ambapo alisema
hawatakuwa na msamaha kwa mwanafunzi atakaye kwenda kinyume na sheria,kanuni na
taratibu walizoweka katika kuhakikisha nidhamu inakuwepo.
Shule hiyo ambayo inamilikiwa na kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa
Victoria Mjini Shinyanga,mbali na kuangalia maadili kwa wanafunzi pia aliwataka
wazazi na walezi kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya watoto wao ili kuona
kama wanapiga hatua.
‘’katika matokea ya kidato cha nne mwaka 2012
wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 61 waliopata daraja la kwanza mpaka
la tatu ni wawili mmoja alienda kidato cha tano,mwaka 2013 kiwango
kilipanda walifaulu 33 kati ya 76waliofanya mtihani,waliofaulu kwenda
kidato cha tano ni 24 tukisimamia maadili ufaulu utaongezeka
zaidi”alisema.
No comments:
Post a Comment