HABARI KAMILI.
WANANCHI wa kijiji cha Bulekela kata ya Masanga wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga wameukataa mradi wa maji ambao umetengewa kiasi cha sh 28.5milion ,kutokana na kutoshirikishwa na wataalamu wakati wakifanya utafiti ,huku wao wakitaka mabomba ya maji yasambazwe karibu na nyumba zao na siyo kuchimbiwa visima virefu au vifupi vya kupampu kwa mkono.
Wakati wananchi hao
wakiukataa mradi huo licha ya kushauriwa na viongozi wakubwa ngazi ya mkoa na
wilaya pasipo kuangalia vijiji vingine wananchi wanakabiliwa na kero kubwa ya
maji, na kumtaka mkurugenzi wa
halmahauri hiyo Jane Mtagurwa kuuhamisha
mradi huo upelekwe sehemu nyingine kwani wao wameonyesha kutouhitaji .
Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri
hiyo diwani wa kata ya Masanga mradi ulipo Shiboka Pombe ,alitoa kilio chake na kusikitishwa na kitendo cha wananchi
kuukataa mradi huo wakati walishirikishwa hatua zote ikiwa ni pamoja na
wataalamu kutoa ushauri kuwa kuweka mabomba haitawezekana kutokana na
utopatikana maji na kushauri kuwachimbia visima viwili maeneo waliyopima na
kuona yanafaa.
“ Zilitengwa jumla ya sh
28.5 milion kwaajili ya kuchimba visima virefu lakini maji
yalipokosekana kwa mujibu wa wataalamu wetu akiwemo mhandisi wa maji Lucas
Saidi, waliamua viwekwe visima vifupi viwili kwa fedha
hizo katika kijiji hicho kimoja ambavyo vitatumia pampu ya mikono”alisema Diwani Pombe.
Akichangia hoja hiyo diwani wa kata ya Mwamashele
Julius Kwihuja alisema maazimio yalikuwa mradi huo
uhamishwe kwani maeneo mengi wananchi wanateseka kwa kukosa huduma ya
maji ,halafu wao wamepata
kiburi kwanini wabembelezwe ni vema ukahamishwa kwani tayari suala
hilo limeshafikishwa kwenye kamati ya
maji na kuzungumzwa kuwa mradi huo uhamishwe kutokana na kujivunia kuwa karibu
na mto.
Hata hivyo mwenyekiti
wa halmashauri hiyo Justine Sheka alisema kuwa utafiti uliopatikana
hapo kuwa eneo hilo maji ni kidogo ila eneo walilochimba kisima maji yapo
kwa wingi ila wao bado hawataki hata mradi ukihamishwa tayari
kunahasara manunuzi ya pambu ni shilingi million saba,gharama ya
uchimbaji shilingi million 20 tayari zimekwisha tumika.
Pia mhandis wa maji
Saidi awali alidai kuwa walipopima eneo hilo walibaini
maji ni kidogo kwa kutotosheleza mtandao wa maji ya pomba kwa kitaalamu
hivyo wakashauri kuwa kuwekwe visima vifupi vya pambu ya mikono
lakini wananchi walipoelezwa walikataa na kutaka mabomba yatakayo sambaaa mpaka
majumbani mwao.
Naye mkurugenzi wa
halmashauri hiyo Jane Mtagurwa alisema kuwa malalamiko yaliyopo
dhidi ya wananchi kuwa wakati wataalamu wanapima hawakushirikishwa ,hivyo
mpango wa upimaji uanze upya kwa kuwashirikisha ikiwa utaratibu wa
kusambaza mabomba ufanyike,wanachokataa kingine ni ile shida ya kupampu
kwa mkono.
“Kuhamisha mradi huo
utaleta tena gharama kubwa hakuna fedha kinachotakiwa ni
kuondoa mgogoro uliopo,mpango wa upimaji uanze upya kwa
kuwashirikisha wananchi na usambazaji wa maji kwenye mambo ufanyike
shida yao hawataki visima hivyo ambavyo vya kupampu kwa mkono ndicho
kilichobainika kwenye kijiji hicho”alisema mkurugenzi Mtagurwa.
Na Stella Ibengwe.
No comments:
Post a Comment