Maafisa wa afya nchini Sierra leone wamethibitisha kwamba mgonjwa mmoja wa Ebola aliyetoroka hospitalini katika mji mkuu wa Freetown amefariki baada ya kurudi hospitalini.
Alijiwasilisha hospitalini humo baada ya serikali kuwataka raia kupitia tangazo la redio kusaidia kumsaka.
Alifariki Wakati alipokuwa akisafirishwa na wazazi wake mashariki mwa Sierra Leone ambapo vituo vya kuwauguza wagonjwa wa Ebola vimejengwa.
Ugonjwa huo umewaua zaidi watu 660 Magharbi mwa Afrika mwaka huu.
Via: bbc swahili.
No comments:
Post a Comment