Monday, June 30, 2014

MIHOGO ,MAGIMBI, VIAZI VYA PANDISHWA BEI SHINYANGA WANANCHI WALIA

Mfanyabiashara wa mihogo katika soko la nguzo nane manispaa ya Shinyanga Mwantumu Almas akiwa na mteja wake Warda Twalibu,akimpa maelezo juu ya kupanda kwa gharama za mihogo na viazi na kusababisha wao kuuza kwa bei ya hasara ambapo fungu moja ni sh 1000 likiwa na mihogo minne hadi mitano. Mwantumu alisema hali hiyo inatokana na wakulima kupandisha bei kutoka sh 8000 hadi 16,000 kiloba kimoja,hivyo kusababisha wao kupunguza idadi ya mihogo kwenye fungu kutoka 8 hadi mitano,ambapo gharama hizo zimepanda baada ya kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Holathi Rwezahura mfanyabiashara wa ndizi katika soko la nguzo  nane manispaa ya Shinyanga akimuuzia mteja wake ndizi,ambapo ndizi nne ni sh 1000 na  mkungu mzima sh 20,000 bei ambayo haijabadilika kama ilivyo kwa vyakula vingine mihogo,viazi na magimbi bei zake ziko juu kutokana na kuanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Balozi wa soko la nguzo nane Hassan Juma ambaye pia ni mfanyabiashara akiwa katika eneo lake la kazi,ambapo alisema changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni kupanda kwa gharama za vyakula hasa mihogo na viazi.
Mfanyabiashara Mwantumu Almas akiendelea na kazi.
Juliana Clement akiweka magimbi kwenye mfuko kwa ajili ya kumpatia mteja wake katika soko la nguzo nane.
Biashara inaendelea  ni mchanganyiko matunda,viazi,mihogo,magimbi na mboga za majani.
Mfanyabiashara Juliana Clement akiwa kazini kwake soko la nguzo nane mjini Shinyanga,anasema kero kubwa iliyopo kwa sasa ni kupanda gharama za magimbi ambapo gunia moja wananunua sh 70,000.
Mfanyabiashara Mwantumu Almas akiwa na wateja wake eneo la biashara soko la nguzo nane mjini Shinyanga.








No comments:

Post a Comment