Mzee Kikongwe aliyefahamika kwa jina moja la Siberi anayetuhumiwa kwa ulozi.
Katika
hali ya kushangaza, mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari amejikuta
kwenye wakati mgumu baada ya kushikana uchawi na kikongwe anayefahamika
kwa jina moja la Siberi akiwa na mganga wake, Rashid na kuibua timbwili
lililotikisa, akimtuhumu kikongwe huyo kumchukua mwanaye kimazingara
‘msukule’.
Tukio
hilo lilitokea wikiendi iliyopita maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala jijini
Dar na kusababisha sekeseke kubwa lililofunga mtaa kufuatia mvutano
ulioibuka baina ya wakazi wa mtaa huo huku baadhi wakiamini ushirikina
wakimhusisha kikongwe huyo.
Mama aliyetajwa kwa jina la Khadija Omari anayemtuhumu mzee huyo.
Kwa
mujibu wa Khadija ambaye ni mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kuchukuliwa
msukule aitwaye Tausi, mwanaye huyo alifariki dunia Agosti, mwaka jana
katika mazingira ya kutatanisha.
Alisema
kifo cha mwanaye kilimtatiza hivyo alikwenda kwa waganga wa jadi
‘kuchungulia’ kama alifariki dunia kweli au ni mauzauza ndipo akabaini
kuwa kikongwe huyo ambaye alikuwa mwenye nyumba wake anahusika.
Mganga akijaribu kutoa dawa ya kurejesha mtoto.
Kufuatia
hali hiyo, Khadija aliamua kuondoka kwenye nyumba ya kikongwe huyo
kwani alikuwa akikutana na mauzauza kila kukicha na kutimkia mkoani
Mwanza huku akijipanga kutafuta mtaalam wa kumtoa mwanaye alipowekwa
msukule.
Alisema hivi karibuni alirejea Dar na kutinga kwa kikongwe huyo akiwa na waganga wa jadi ili kumpata mwanaye.
Baadhi ya mashuhuda waliofika kushuhudia sekeseke hilo.
Hata
hivyo, zoezi hilo halikufanikiwa baada ya ndugu wa kikongwe huyo
kuingilia kati na kuanzisha timbwili la aina yake wakimtetea kwa madai
hawana imani kama anajihusisha na vitendo vya aina hiyo.
No comments:
Post a Comment