Wawakilishi wa Abdulah wanadai udanganyifu unaendelea
Waendeshaji kampeni za mojawapo
wa wagombea urais nchini Afghanistan Abdullah Abdullah wamesusia ukaguzi
wa kura leo, wakisema matakwa yao ya kusitisha udanganyifu
hayajatimizwa.
Ukaguzi kamili wa kura hizo zilizopigwa
kumtafuta atakayemrithi rais Hamid Karzai umekuwa ukiendelea kwa zaidi
ya mwezi mmoja sasa.
Shughuli ya Ukaguzi wa Kura umeendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja
Lakini wakati ukaguzi wa kura hizo ulipoingia awamu yake ya mwisho wiki hii, huku maboxi kadhaa pekee ndiyo yaliotupwa, kundi la Abdullah wamesema watasusia shughuli hiyo.
Linaamini kwamba malefu ya kura zilipigwa katika duru ya pili ya uchaguzi hu kwa mgoombea aliyeongoza katika uchaguzi huo unaokumbwa na mzozo wa hesabu ya kura, Ashraf Ghani.
Viongozi wanaowania Urais nchini Afghanistan walipokutana na Jonh Kerry
Huu unaonekana kama wakati hatari mno kaika nchi ambayo madaraka yamebadilika miongoni mwa watu kwa kutishiwa kwa mtutu wa bunduki.
Baadhi ya wafuasi wa Abdullah wametishia kufanya maandamano barabarani iwapo shughui hiyo ya kuheabu upya kura haitofanyika kwa usawa.
VIA: BBC.
No comments:
Post a Comment