Sunday, November 23, 2014

KUKU WATUMIKA KUHAMISISHA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA CHF

 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Gimagi kata ya Shagihilu wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga wakijiandikisha kwa wataalamu wa afya kwa  ajili ya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF zoezi ambalo linaratibiwa na mfuko wa
bima ya afya mkoa wa Shinyanga,ambapo katika vijiji viwili vya Mwalata na Gimagi katika mikutano ya hadhara iliyofanyika kwa nyakati tofauti wakati wa uzinduzi wa mfuko huo jumla ya kaya 107 zilijiunga na mfuko wa afya ya jamii kwa sh 5000 tu wanatibiwa bure watu nane katika familia mwaka mzima kwenye  vituo vya afya,zahanati na hospitali za serikali zilizopo ndani ya wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya kishapu Wilson Nkhambaku akiwahamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF ili wapatiwe matibabu bure mwaka mzima kwa kulipia Sh 5000,katika  kutoa elimu alilazimika kutumia mfano wa kuku kuwa ukiwa naye mmoja ukimuuza unaweza kulipia fedha hiyo na bado ukabaki na chenji na kuwataka kubadilika kwani mambo yanabadilika kila wakati .
Wanakwaya wa kijiji cha Mwalata akicheza pamoja na  mkuu wa wilaya hiyo Wilson Nkhambaku,wakati wa uzinduzi wa mfuko wa  CHF katika kata ya Shagihilu.
Wananchi wa kijiji cha Mwalata wakiwa  kwenye mkutano
Mkutano  unaendelea.








No comments:

Post a Comment