Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindayi ambaye ni mwenyekiti wa wenyeviti
nchini akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wenzake baada ya mazishi ya
mama mzazi wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja(Bi Halima
Nchimika).Picha na Kadama Malunde
Waziri
mkuu wa zamani Edward Lowassa amemtumia salamu za rambirambi mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja baada ya kufiwa
na mama yake mzazi Halima Nchimika(74) wakati akipatiwa matibabu katika
hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Halima
Nchimika aliyezaliwa mwaka 1940 alifariki dunia Novemba 18 mwaka huu
katika hospitali ya rufaa ya Bugando baada ya kuugua kwa muda mrefu na
mazishi yake yamefanyika Novemba 19,2014 katika makaburi ya Uhindini
mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Akitoa
salamu za rambirambi baada ya mazishi kwa niaba ya mbunge wa Monduli
Edward Lowassa(waziri mkuu mstaafu),mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
mkoa wa Singida Mgana Msindayi ambaye pia ni mwenyekiti wa wenyeviti wa
mikoa wa CCM alisema Lowassa amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha
Halima Nchimika.
Katika
salamu hizo na pole Lowassa alisema alimfahamu vyema marehemu na kwamba
siku za nyuma aliwahi kuishi nyumbani kwa Mgeja akabahatika kupata
wosia kutoka kwa mzee huyo na kupiga naye picha mbalimbali za ukumbusho.
“Ndugu
yetu Lowassa kanituma nifikishe ujumbe huu,yeye yuko nje ya nchi
anawapa pole sana familia ya marehemu,Lowassa aliwahi kuishi hapa kwa
Mgeja,anamjua vyema mama yetu aliyetutoka,anawaomba wanafamilia muwe na
subira kwa ni mipango ya mungu”,aliongeza Msindayi.
Kwa
upande wake mbunge wa jimbo la Kahama Mjini James Lembeli alisema
Halima Nchimika alikuwa mtu mwema hivyo kumuasa mtoto wa marehemu Khamis
Mgeja kuishi maisha aliyokuwa anaishi mama yake.
“Namfahamu
vyema mama huyu ndiyo sababu kubwa ya mimi kufika hapa,alikuwa mtu
mwema,pengine hata hii mvua iliyonyesha baada ya kumsitiri mama
yetu,watumishi wa mungu mtanisamehe,hii maana yake mwenyezi mungu
kampokea huyu mama”,alisema Lembeli.
“Siyo
rahisi mtu anazikwa mvua ikanyesha,huyu mama mvua imenyesha,ndugu yangu
Mgeja naomba uishi kama alivyoishi mama yako,umati huu siyo
bure,alikuwa mama wa watu,nawashukuru viongozi wote mliofika hapa,naomba
tuendelee kumwombea mama yetu ili mwenyezi mungu ampokee”,aliongeza
Lembeli.
Naye
Shehe wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya alitaka jamii kutenda
mambo mema na kusaidia na kuwapenda wazazi kwani baraka nyingi zinatoka
kwa wazazi katika maisha ya mwanadamu.
Akitoa
neno la shukrani kwa niaba ya familia yake,mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Shinyanga Khamis Mgeja aliwashukuru mamia ya watu waliojitokeza wakiwemo
viongozi wa serikali,siasa,dini,waandishi wa habari na watu wote kutoka
ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga waliojitokeza kumfariji katika msiba
huo mzito kwake.
Hata
hivyo katika hali ya kushangaza wakati mwili wa marehemu ukitolewa
nyumbani kwao mtaa wa Nyasubi mjini Kahama kuelekea katika msikiti mkuu
wa Ijumaa kuswaliwa mvua ilianza kunyesha kisha kukatika na wakati
mazishi yakimalizika katika makaburi ya Uhindini mjini Kahama ghafla
mvua ilianza kunyesha ikakatika baada ya msafara kufika nyumbani.
|
No comments:
Post a Comment