Tuesday, November 18, 2014

TASAF AWAMU YA TATU YAJA NA MKAKATI WA KUNUSURU KAYA MASIKINI

Watumishi wa halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa  wa TASAF wakati wa mafunzo ya mpango wa kuzinusuru  kaya masikini.

Mwakilishi wa mkurugenzi wa TASAF Alphonce Kialiga akizungumza  na watumishi  hao,ambapo aliwataka kusimamia kikamilifu mpango huo ili  uwafikie walengwa.
Maafisa wawezeshaji kutoka kata mbalimbali.

Msimamizi wa mpango wa TASAF awamu ya tatu  kanda ya kati Barnabas  Mkumbo aliwataka madiwani kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo, kwa kuhakikisha kaya zote zitakazo ingizwa kwenye mpango  zinazingatia mashariti yaliyowekwa ili kuendelea kupata ruzuku zitakazotolewa.

Mafunzo yanaendeea
Katibu tawala wa wilaya hiyo Julias Samweli akiwataka  watendaji kuhakikisha wanatumia fursa hiyo vizuri,hatua itakayosaidia kuchochea maendeleo kwenye wilaya  hiyo na mkoa mzima kwa ujumla sanjari na kaya masikini kuwa na uhakika wa kipato kupitia shughuli mbalimbali watakazofundishwa.





No comments:

Post a Comment