Tuesday, November 18, 2014

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AJIUA BAADA YA KUKATAZWA KUUZA NGOMBE WA BABA YAKE.

NZI AJINYONGA HADI KUFA BAADA YA KUNYIMWA KUUZA NG'OMBE WA BABA YAKE

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Nyandoto Wilayani Tarime Peter Mwikabwe mwenye miaka19  amekutwa Amekufa kwa kujinyonga kwa kamba nyumbani kwao baada ya kuzuiwa kuuza ng’ombe wa baba yake .
Baba wa mwanafunzi huyo alisema mtoto wake alikwenda kwa ndugu yake na kumdanganya kuwa ametumwa achukue ngo’ombe amuuze kwa aji ya mahitaji ya shule lakini kabla hajapewa ngo’ombe hao walipiga simu nyumbani kwao kutaka kupata ukweli ndipo ikagundulika alidanganya na kunyimwa.
Baada ya kumkataza kutaka kuuza ngo’mbe kijana wake aliingia chumbani na walidhani amekwenda kulala lakini baada ya kimya cha muda mrefu waliingia chumbani kwake na kumkuta ananing’inia na kamba akiwa tayari amefariki.
Kamanda wa Polisi Tarime Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwaasa vijana kuachana na tabia za kukimbilia maisha ya starehe ambayo hayana faida kwao.
Via Eddy  blog

No comments:

Post a Comment