Friday, November 14, 2014

YALIYOJIRI SHINYANGA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI

Leo  Novemba 14,ni siku ya maadhimisho ya siku ya kisukari,ambapo katika mkoa wa Shinyanga yanafanyika katika hospitali ya rufaa ya mkoa.Elimu juu ya ugonjwa huo inatolewa na wananchi wanapima afya zao kujua kama wana ugonjwa wa kisukari ama la!
Mratibu wa kisukari mkoa wa Shinyanga Ruth Kanoni akitoa elimu kwa wakazi wa Shinyanga kuhusu ugonjwa wa kisukari ambapo amewataka kujiepusha na ulaji wa nyama kupita kiasi kwani ina mafuta yanayoganga mwilini na kumfanya mtu awe hatarini kupata magonjwa ikiwemo kisukari,moyo.Pia amesema ni vyema wananchi wakala vyakula vya nafaka,mizizi na ndizi kwa uangalifu na kula makapi ya nafaka ili kusaidia kutonenepa na kula sana matunda sambambamba na mbogamboga na kuepuka vyakula vya mafuta
Wananchi wakifuatilia kinachoendelea katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga
 Mratibu huyo wa kisukari mkoa wa Shinyanga Ruth Kanoni amewaasa wananchi kuepuka kunywa pombe,soda na juisi
 na kuvuta sigara

Pichani ni Mary Clement ambaye ni mhudumu wa afya katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga akitoa huduma kwa mmoja wananchi wa mkoa wa Shinyanga waliofika katika maadhimisho ya siku ya kisukari leo katika hospitali hiyo 
Takwimu zinaonesha kuwa wagonjwa wa kisukari wanazidi kuongezeka mkoani Shinyanga ambapo hospitali ya mkoa wa Shinyanga kila wiki inapokea wagonjwa wa kisukari wanne hadi watano

Hata hivyo imeelezwa kuwa wanawake ndiyo wanaongoza kwa kupima afya zao tofauti na wanaume ambapo mratibu wa kisukari mkoa wa Shinyanga Ruth Kanoni ametumia fursa hiyo kuwataka wanaume kubadilika na kujenga tabia ya kupima afya zao
Sababu zilizotajwa kuchangia kuwepo kwa ugonjwa wa kisukari ni tabia za kimaisha ikiwemo kula na kunywa kupita na kutofanya mazoezi

No comments:

Post a Comment