Sherehe zinatarajiwa kuanza muda mfupi unaokuja nchini Ujerumani za kuadhimisha miaka 25 tangu kuanguka kwa ukuta wa Berlin.
Kuanguka kwa ukuta huo kulichangia kumalizika kwa vita baridi na kusaidia kuliunganisha taifa la ujerumani.
Sherehe mbali mbali zitaandaliwa huku chansela wa ujerumani Angela Merkel akiweka shada la maua na kuhudhuria ibada kanisani kuwakumbuka waathiriwa wa utawala wa kikumunisti kwenye iliyokuwa ujerumani mashariki.
Merkel ataungana na aliyekuwa kiongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini Poland Lech Walesa pamoja na kionngozi wa zamani wa uliokuwa muungano wa usovieti Mikhail Gorbachev.
No comments:
Post a Comment