Sunday, November 9, 2014

MWALIMU AJIFICHA SHIMONI NI BAADA YA KUSABABISHA KIFO CHA MWANAFUNZI KWA VIBOKO


Mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya msingi ya Kiuu Kenya amefariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu wake kwa kufeli somo lake la Kiswahili. 
 
Familia ya mtoto huyo Joseph Waburi mwenye umri wa miaka kumi imesema mtoto huyo alikuwa na nidhamu ya hali ya juu.
 
Mama wa mwanafunzi huyo Grace Muthoni amesema mtoto wake alienda shule Jumatatu asubuhi na aliporudi alianza kulalamika maumivu ya kichwa na shingo, siku iliyofuatia alimpeleka Zahanati ya Wilaya ya Nyagiti level 4.
 
Siku ya pili alilazimika kumrudisha Hospitali baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, daktari akashauri ahamishiwe katika Zahanati ya Muran’ga Level 4 kwa matibabu zaidi.Wakati akisubiri gari la wagonjwa akafariki dunia.
 
Mama huyo amesema uchunguzi wa awali unaonyesha mtoto wake alipigwa na Mwalimu na kupata majeraha kichwani na shingoni, mwili wake umehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi kubaini sababu za kifo chake.
 
Mwalimu anayedaiwa kumpiga Mwanafunzi huyo alikimbia kujificha shimoni baada ya kusikia taarifa za kifo, huku Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Joseph Mwenda akikanusha uvumi kwamba mtoto huyo alifia shuleni.

No comments:

Post a Comment