Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya walaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani katika ukumbi wa halmashauri hiyo, ambapo suala la bei ya mbegu za pamba zilizua mjadala mkubwa huku
wakitaka iundwe kamati ya kwenda wizara ya kilimo chakula na ushirika kufuatilia hatima ya zao hilo kutokana na bei yake kutoeleweka kila msimu na kutaka kupatiwa majibu ya kina, kwani wakulima hawana faida na kilimo hicho ikiwa ni pamoja na mbegu za pamba kupandishwa bei kutoka sh 300 hadi 500 kwa kilo moja sawa na yanavyonunua makampuni jambo ambalo linawaumiza wakulima hali ambayo imesababisha baadhi yao kupalilia magugu ya zao hilo (maotea) shambani badala ya kuyakata. |
No comments:
Post a Comment