Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures iliyopo katika eneo la Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga wametembelea kituo cha walemavu wa ngozi (Albino) cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo mchele,pipi,biskuti,sukari,chumvi,nguo,mafuta ya kujipaka
Stella Blog
Thursday, August 11, 2016
WANAFUNZI SHULE YA LITTLE TREASURES WAWATEMBELEA WAZEE,ALBINO NA WAGONJWA
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures iliyopo katika eneo la Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga wametembelea kituo cha walemavu wa ngozi (Albino) cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo mchele,pipi,biskuti,sukari,chumvi,nguo,mafuta ya kujipaka
Wednesday, March 11, 2015
WATU ZAIDI YA 30 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI MBAYA BAADA YA BASI LA ABIRIA KUANGUKIWA NA KONTENA HUKO IRINGA
Tunafuatilia
kwa karibu taarifa ya ajali mbaya sana ambayo imetokea eneo la
Changalawe, Mafinga, mkoani Iringa basi la Majinja toka likitokea Mbeya
kwenda Dar es salaam limeangukiwa na kontena na taarifa zisizo rasmi
zinasema abiria wengi wamepoteza maisha yao.
Thursday, December 18, 2014
PROFESA TIBAIJUKA ASEMA KAMWE HAWEZI KUJIUZURU WADHIFA WAKE.
Siku Moja baada ya kujiuzuru kwa Mwanasheria
mkuu Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani
na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake
kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa
mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi jijini
Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa
shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya
kufanya hivyo kwani kufanya hivyo ni kukubali kuwa amehusika moja kwa
moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.
Profesa Tibaijuka amekwenda mbali zaidi na kusema
kuwa uvumi unaoendelea kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani
unawaaminisha wananchi kuwa amehusika katika sakata hilo wakati yeye
hajahusika na jambo lolote.
Via :Mwananchi.
Via :Mwananchi.
ALALA BARABARANI KUCHANGISHA FEDHA KUMSAIDIA MWANAUME ASIYEKUWA NA MAKAO
Mwanafunzi
anayesoma katika chuo kikuu cha Lancashire nchini Uingereza amekuwa
akilala katika barabara za mji wa Preston ili kuchangisha fedha za
kumsaidia mwanamume
Wednesday, December 3, 2014
HAYA NDIYO YALIYOJIRI SHINYANGA MKUTANO WA MWIGULU NI BAADA YA KUAPISHA MAKAMANDA
Thursday, November 27, 2014
MTOTO WA SHULE YA AWALI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI CHENYE FUTI 50
Kisima
chenye urefu wa futi 50 ambapo mtoto Mack Johnson amefariki dunia baada ya
kutumbukia, Mtoto huyo mwenye umri wa miaka (5)alikuwa anasoma darasa la awali katika shule ya Sheer Bliss
mtaa wa majengo mapya manispaa ya Shinyanga. Ambapo ngazi mbili za jeshi la zimamoto pamoja na kuungwa lakini
hazikuweza kufikia kina cha kisima hicho na badala yake ikatumika kamba ndefu
na mmoja wa wananchi kujitoa mhanga kutumbukia nayo kisimani kuutoa mwili wa
mtoto huyo.
Mashuhuda wamesema tukio hilo limetokea leo saa tatu asubuhi ambapo mtoto huyo alitumbukia
kwenye kisima hicho wakati akicheza na wenzake karibu na kisima hicho kilichopo eneo la shule ambacho
kimefunikwa na makaravati yaliyoonekana kuchakaa.
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa eneo la tukio Dkt Anselm Tarimo amesema wamebaini kuwa mazingira ya shule hiyo siyo rafiki, shimo lilikuwa halijafunikwa hivyo kuwaomba wataalam mbalimbali wawe wanapita katika maeneo wanakosomea watoto ili kujua mazingira ya watoto kuepusha majanga yanayoepukika.
Mwili wa
mtoto Mack Johnson ukitolewa kwenye kisima cha maji na wananchi
waliofika eneo la tukio wakishirikiana na jeshi la wananchi na jeshi la zimamoto
na uokoaji.
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa eneo la tukio Dkt Anselm Tarimo amesema wamebaini kuwa mazingira ya shule hiyo siyo rafiki, shimo lilikuwa halijafunikwa hivyo kuwaomba wataalam mbalimbali wawe wanapita katika maeneo wanakosomea watoto ili kujua mazingira ya watoto kuepusha majanga yanayoepukika.
BARIDI YAGANDISHA BREKI ZA NDEGE ABIRIA WALAZIMIKA KUSHUKA NA KUISUKUMA
Abiria
waliokuwa wanafanya safari na shirika ka ndege la Serbia walilazimika
kushuka katika ndege hiyo na kuisukuma baada ya breki zake kuganda na
kushindwa kuondoka.
Subscribe to:
Posts (Atom)