Tuesday, July 1, 2014

POLISI SHINYANGA YAADHIMISHA SIKU YAO MAALUM ,MAPYA YAIBUKA FUATILIA TUKIO ZIMA HAPA

 
Wadau wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa katika ukumbi wa Karena hotel,ambapo imefanyika warsha ya kuwakutanisha wadau hao ikiwa ni siku maaum ya polisi mkoa wa Shinyanga .                                                                                                              Katika warsha hiyo jeshi la limewataka wadau kushirikiana kuwafichuwa wahalifu kwa kuwa  wanaofanya vitendo hivyo ni miongoni mwa wanajamii  hivyo ushirikiano ukiwa imara na kuwatumia polisi jamii uhalifu unaweza kuisha.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya akizungumza na wadau wa jeshi la polisi,alisema licha ya vitendo vya uhaifu kupungua katika mkoa huo lakini bado kunachangamoto kubwa ya ukosefu wa elimu kwa baadhi ya wananchi kwa kuendelea kuamini imani za kishirikina ambazo zimekuwa zikisababisha mauaji ya vikongwe wasiokuwa na hatia.           Kihenya alisema elimu bado ni changamoto kubwa kutokanan na watu kushindwa kwenda hospitali na kuamini waganga wa kienyeji ambao baadhi yao wanapiga ramli chonganishi na kusababisha watu kuuwana na aliwataka wadau hao kila mmoja kutumia nafasi yake kukemea hali hiyo.
Wadau wakimsikiliza kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya,wadau hao ni wafanyabiashara,viongozi wa vyama vya siasa,dini,mashirika na viongozi wa serikali.
Naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika warsha hiyo ,ambapo alisema maboresho ya jeshi la polisi yanayoendelea nchini yanasisitiza juhudi za dhati za  kupambana na ukiukwaji wa maadili ndani ya jeshi hilo ili kuimarisha huduma bora kwa wateja na kuwataka askari kuzingatia maadili ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitndo vya rushwa ambavyo vinachafua sifa ya utendaji kazi wa jeshi.
Wadau wakiendelea kusikiliza ufafanuzi uliokuwa ukitolea na viongozi kwenye warsha hiyo.
Mkuu wa tathimini na ufuatiiaji wa jeshi la polisi nchini Naibu kamishina Marco Gyumi akizungumza na wadau hao ,alisema kwa sasa wafanyabiashara wanapaswa kubadilika na kuhakikisha wanafunga CCTV Camera katika maeneo yao ya biashara na kuwa tayari kuziunganisha kimtandao na control room ya polisi ili kutoa msaada wa kuzuia na kutanzua mapema uhalifu utakaojitokeza.


Viongozi wa jeshi la polisi wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wengine wa jeshi hilo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akichangia mada katika warsha hiyo juu ya ulinzi shirikishi,ambapo alisema hakuna umuhimu wa kuwa na askari kata wakati hawakai katika maeneo yao ya kazi hata tukio la uhalifu likitokea wananchi wanakosa msaada wa polisi na kulitaka jeshi hilo kuhakikisha askari wote wa kata wanakaa maeneo yao ya kazi kwani wapo kwa ajili ya kusaidia jamii na siyo kukaa makao makuu ya mji.


Warsha inaendelea
Wadau wa jeshi la polisi wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Warsha inaendelea
Aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga (RCO)Hussein Kashidye ambaye kwa sasa amehamishiwa makao makuu ya jeshi ,akitoa shukrani kwa wadau wa jeshi hilo kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi chote alipokuwa RCO wa mkoa huo.Aliwataka kuendelea kukemea vitendo vya ukatili kwa watoto,wanawake na mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina.
RCO wa mkoa wa Shinyanga  Mussa  Athuman ambaye amechukuwa nafasi ya Hussein Kashindye aliyehamishiwa makao makuu ya jeshi la polisi akizungumza na wadau ikiwa ni siku maalum ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga.
Waandishi wa habari na wadau wengine wa jeshi la polisi wakiwa katika ukumbi wa karena hotel kwenye warsha iliyoandaliwa na jesi hilo.
 









No comments:

Post a Comment