Tuesday, August 26, 2014

ASKOFU WA KANISA LA EAGT ABURUZWA MAHAKAMANI NA WAUMINI WAKE

 Waumini wa kanisa la EAGT Majengo mjini Shinyanga wakiwa katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga wakiwa wameshikilia mabango



Kesi inayomkabili Askofu wa Kanisa la (EAGT) , kanda ya Magharibi Rafaeli Machimu,Dhidi ya waumini wa dhehebu hilo lililopo Majengo Mjini Shinyanga ,kwa madai ya kuwanyanyasa kwa kumfukuza Mchungaji wao David Mabushi bila kosa lolote ambaye bado wanamuhitaji imeanza kusikilizwa mahakamani.
Kesi hiyo imeanza kusikilizwa jana katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga,lakini mahakama imeahirisha shauri la kesi hiyo, lililofunguliwa na waumini baada kuona upande wa mlalamikaji haukukidhi vigezo vya sababu ya kufungua shauri hilo.
Akisoma shauri la kesi hiyo  hakimu mwandamizi wa wilaya Thomson Mtani katika mahakama hiyo alisema mahakama imeona kwa upande wa mlalamikaji kuwa shauri dogo namba 08/2014 lililofunguliwa kupitia kwa mwanasheria Norbat Beda halina sababu ya kufunguliwa kwake.
Hakimu Mtani alimuomba wakili wa upande wa mlalamikaji Norbat Beda aandike upya sababu za msingi za kufungua kesi hiyo, ili wakili wa upande wa pili wa mlalamikiwa Bartazar Mwairo aweze kujibu haraka shtaka hilo dhidi ya mteja wake siku ya kesi iliyopangwa kusikilizwa tena Agoust 28 mwaka huu.
Shauri hilo lililokuwa linapinga kitendo cha Askofu wa kanisa la EAGT kanda ya Magharibi kumwandikia barua ya kumfukuza mchungaji Mabushi katika kanisa hilo itasomwa tena agosti 28 mwaka huu
Kesi hiyo ilianza kutajwa tarehe 4 Agosti ,2014, katika mahakama ya wilaya  na mara ya pili ilisikilizwa Agosti 14, na kuahirishwa kusikilizwa kwa sababu wakili wa mshitakiwa aliiomba mahakama iahirishe kusikilizwa kutokana na kutoelewa kina cha kesi hiyo hivyo ilitarajiwa kusikilizwa tena  Agosti 25 imeahirishwa tena mpaka Agosti 28 mwaka huu.
Waumini wa kanisa hilo walimfikisha mahakamani Askofu Rafael Machimu Agost 4 mwaka huu, kwa madai ya kuwanyanyasa kwa kuwafukuza mara kwa mara wachungaji wa kanisa lao la( EAGT),la Majengo Mjini Shinyanga bila ya Sababu za msingi.

Walisema kanisa hilo lilianzishwa mwaka 1992 likiwa chini ya mchungaji John Chambi ambaye aliondolewa na uongozi wa jimbo la Shinyanga akiwepo mchungaji Rafael Machimu ambaye wakati huo alikuwa katibu wa jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment