Thursday, August 21, 2014

HAYA NDIYO YALIYOJIRI WILAYANI KAHAMA LEO ONA TUKIO ZIMA HAPA.



Mwezeshaji wa mafunzo ya Tohara ya wanaume kitaifa kutoka wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Dkt Nicholaus Mbassa wakielekezana kuhusu tohara ya wanaume na mwandishi wa Itv/Radio one bwana Stephen Wang'anyi baada ya mafunzo hayo katika siku ya kwanza kumalizika leo.

Hapa ni ndani ya ukumbi wa Cartas mjini Kahama mkoani Shinyanga ambako leo  waandishi wa habari wameanza kupatiwa mafunzo ya siku 2 kuhuhu mradi wa Tohara kwa wanaume  kwa ajili ya kukinga maambukizi ya VVU,katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu na wilaya ya Rorya mkoani Mara wa kwanza ni Greyson Kakuru mwandishi wa habari TBC,akifuatiwa na Raymond Mihayo mwandishi wa habari gazeti la Habarileo akifuatiwa na Stephen Wang'anyi mwandishi wa habari ITV/Radio one.Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirika la Intrahealth  International yanalenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuripoti habari zinazohusu Tohara kwa wanaume
Mwezeshaji wa mafunzo ya Tohara ya wanaume kitaifa kutoka wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Dkt Nicholaus Mbassa akionesha mfano wa uume.Alisema mwanamme ambaye hajafanyiwa tohara akifanya ngono na mwanamke mwenye maambukizi ya VVU,yuko hatarini kuambukizwa VVU mara 7 zaidi na kwamba endapo mwanamme akifanyiwa tohara kuna uwezekano wa hadi asilimia 60 kutoambukizwa VVU,hivyo kuwataka wale ambao hawajafanyiwa tohara kufika katika vituo vya afya kwani huduma hiyo inatolewa bure
Kushoto ni Raymond Mihayo mwandishi wa habari gazeti la Habarileo kulia kwake ni Stephen Wang'anyi mwandishi wa habari wa ITV/Radio one wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini 
Kushoto ni afisa habari kutoka Intrahealth International bwana Mkama Mwijarubi,kulia kwake ni Afisa mradi wa Tohara ya wanaume kutoka Intrahealth International  Dr Innocent Mbughi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.Pamoja na mambo mengine Dkt Nicholaus Mbassa alisema mbali na kukinga maambukizi ya VVU kwa 60%,Tohara pia inasaidia mwanamme asimwambukize mkewe saratani ya shingo ya uzazi.

Mwezeshaji wa mafunzo ya Tohara ya wanaume kitaifa kutoka wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Dkt Nicholaus Mbassa aliwaomba viongozi wa siasa,dini,wanahabari jamii hususani akina mama kuwahamasisha wanaume kufanyiwa tohara kwani ina faida nyingi kama vile kukinga maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono ,kukinga maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi,usafi kwa wanaume n.k

Afisa mradi wa Tohara ya wanaume kutoka Intrahealth International  Dr Innocent Mbughi akieleza mafanikio ya shirika hilo ambapo alisema tangu mwaka 2011 hadi sasa jumla ya wanaume 295,231 kutoka mikoa ya Simiyu,Shinyanga na wilaya ya Rorya wamefanyiwa tohara kupitia mradi wa shirika hilo kwa kushirikiana na serikali.Alisema huduma hiyo inatolewa bure katika vituo mbalimbali Mkoani Shinyanga ni  Hospitali ya wilaya ya Kahama,Kituo cha afya Lunguya,Ushetu,Nindo,Songwa,Kishapu,hospitali ya mkoa wa Shinyanga.Mkoani Simiyu ni kituo cha afya Busega(Nasa),hospitali ya Mkula,hospitali ya wilaya ya Maswa,Bariadi na Meatu na mkoani Mara wapo katika wilaya ya Rorya katika kituo cha afya Shanguge na Utegi
Mwandishi wa habari Gazeti la Nipashe/Radio Faraja bwana Michael Maduhu akifuatilia kilichokuwa kinajiri kuhusu umuhimu wa tohara ya wanaume
Kulia ni  Raymond Mihayo mwandishi wa habari gazeti la Habarileo akiuliza swali wakati wa semina hiyo leo
Afisa habari kutoka Intrahealth International bwana Mkama Mwijarubi akizungumza katika semina hiyo ambapo alisema wanaume wengi hawajitokezi kufanyiwa tohara kutokana na kukosa uelewa wa kutosha kuhusu tohara na wengine kuwa na aibu ,huku wale wenye umri kuanzia miaka 35 wakidai kuwa muda wa kufanyiwa tohara umepita.Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanaume wote kujitokeza kupata huduma hiyo

Kushoto ni mkurugenzi wa Malunde1 blog bwana Kadama Malunde,anayeandikia pia gazeti la Zanzibarleo kulia kwake ni bwana Shija Felician mwandishi wa habari gazeti la Mwanachi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri

Msimamizi wa kituo cha huduma ya Tohara ya wanaume wilaya ya Kahama ndugu Masaga Odhiambo akiwa katika ukumbi wa Cartas mjini Kahama wakati wa semina kwa waandishi wa habari,iliyoandaliwa na Intrahealth International
Mwandishi wa habari kutoka radio Kahama Paulina Juma akifuatilia kilichokuwa kinaendelea,ambapo wanawake waliaswa kuwashauri waume zao kupata huduma ya tohara kwani mwanamme ambaye hajafanyiwa tohara anaweza kusababisha maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi

Picha zote na Kadama Malunde na Michael Maduhu-Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment