Wednesday, August 27, 2014

HUU NI UKATILI WA KINYAMA ALIOFANYIWA MTOTO HUYU WA DARASA LA TATU

Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila akishiriki mazishi ya mwanafunzi wa darasa la tatu Happness Kashindye miaka (9) mkazi wa negezi kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga ,ambaye alikutwa amekufa baada ya kubakwa na kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani.

Safari ya mwisho ya mtoto Happiness Kashindye mwenye umri wa miaka 9 aliyeuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.Pichani ni jeneza lililobeba mwili wa marehemu wakati wa shughuli za mazishi yaliyofanyika leo mchana katika makaburi ya familia katika kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza katika manispaa ya Shinyanga.

Mtoto Happiness Kashinje enzi za uhai wake
Wananchi wenye mapenzi mema wakiwa eneo la makaburini leo
Wanafunzi wa  shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga wakishiriki shughuli za mazishi ya mwanafunzi mwenzao aliyeuawa kinyama
 Walimu wa shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga wakishiriki shughuli za mazishi ya mwanafunzi wao
Baba mzazi wa mtoto Happiness Kashinje bwana Kashinje Mayala akizungumza na malunde1 blog baada ya mazishi ya mtoto wake kipenzi kuhusu tukio hilo ambapo alisema mwanaye alikuwa anaishi na shangazi  yake Mahegi Mayala na aliaga kwenda kunyoa nywele saluni majira ya saa tisa alasiri siku ya Jumapili na baada ya hapo hakurudi tena nyumbani.

Mayala alisema siku ya Jumatatu walipata taarifa kuwa kuna mtoto ametupwa kwenye vichaka karibu na Shamba la Mwandu Misona na walipofika eneo la tukio hawakumkuta mtoto huyo na kudaiwa kuwa amepelekwa na wasamaria wema katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Alisema kufuatia taarifa hizo aliamua kuufuatilia mwili huo hospitalini hapo ,ili kuweza kubaini kama ni mtoto wake na alipofika katika chumba cha kuhifadhia maiti alibaini mwili huo kuwa ni wa mtoto wake Happiness Kashinje.

No comments:

Post a Comment