Rubani
wa kwanza wa kike nchini Kenya sasa amepata mafanikio zaidi kwa kufuzu
kuwa rubani wa kwanza mwanamke barani Afrika kushika usukani wa ndege za
kisasa aina ya Boeing 787 Dreamliner.
Imemchukuwa
Rubani Irene Koki Mutungi kipindi cha zaidi ya miaka ishirini
kufanikiwa kuvunja pingamizi zote zinazowazuia wanawake kuingia katika
taaluma hiyo inayotawaliwa na wanaume.
Mwandishi wa BBC Denis Okari alifanikiwa kukutana naye baada ya kutua
kutoka ndege hiyo ambayo ni ya nne katika msafara wa ndege mpya aina ya
Dreamliner zinazomilikiwa na shirika la ndege la Kenya Airways.kwa
kipindi kirefu-Rubani huyo ambaye sasa amepewa jina la Boeing Girl
anasema mambo bado.
Hamu ya kuwa rubani kwa Koki ilitokana na kazi ya babake ambaye pia alikuwa rubani
Koki alikuwa mwanamke wa kwanza rubani kufanya kazi katika shirika la ndege la Kenya kwa miaka sita.
Alianza kazi yake ya kuendesha ndege mwaka 1993.
Kazi
yake ya kwanza hata hivyo ilikuwa aliposhika usakani wa ndege ya Fokker
50 kwenda Kisumu Magharibi mwa Kenya kama kazi ya kwanza ya kulipwa.
Alianza kupenda kuendesha ndege alipokuwa msichana mwenye umri wa miaka 17.
Babake
Koki pia ni rubani. Yeye ndiye alimfanya mwanawe kupenda kuendesha
ndege. Alianza kufurahia kazi hiyo kila alipomuoana babake akiifanya na
hapo ndipo akaamua naye kwamba siku moja atakuwa rubani kazi inayofanywa
zaidi na wanaume.
Alianza masomo yake katika chuo cha mafunzo ya uendeshaji ndege cha Oklahoma nchini Marekani.
Anasema
angependa zaidi kuwasaidia wasichana wengine wa kiafrika na pia
kuanzisha wakfu wake wa kuwasaidia watu masikini katika jamii.
No comments:
Post a Comment