Friday, August 22, 2014

MWENYEKITI WA MTAA WA MAJENGO MAPYA KUPITIA CCM AJIUNGA NA CHADEMA.

 Mwenyekiti  wa Chadema  Shinyanga mjini Hassan Baruti akimtambulisha aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa wa majengo mapya manispaa ya Shinyanga kupitia CCM Damari Nyantabano, ambaye ameamua kujiuzuru wadhifa huo na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Nyantabano alisema hatua ya kujiuzuru ni kutokana na kuchoshwa na ukilitimba wa chama hicho, ambacho kimekuwa kikiwa nyanyasa viongozi wake kwakuwapelekesha na kuwataka wafanyekazi kama wanavyotaka wao bila ya kuzingatia maslahi ya wananchi.
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama taifa (Chadema),Wilfred Lwakatare akimpongeza Damari Nyantabano ambaye alikuwa mwenyekiti wa mtaa wa majengo baada ya kujiunga na CHADEMA ,ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wakazi wa manispaa ya Shinyanga kutofanya makosa kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu (2015),kwa kuchagua viongozi wasiojali maslahi yao.
Rwakatare alisema kwa miaka mingi wamekuwa wakifanya makosa kwenye Chaguzi kuanzia Serikali za mitaa hadi uchaguzi kuu kwakuchagua viongozi wasio na maslahi kwao na kuufanya mjini huo kuwa nyuma kimaendeleo huku akisisitiza kuwa UKAWA hawatarudi bungeni mpaka suluhisho litakapopatikana.









na.

No comments:

Post a Comment