Rais wa Liberia Ellen Johnson
Sirleaf ametangaza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku kuanzia saa
tatu hadi saa kum na mbili asubuhi.
Watu hawataruhusiwa kuingia au kutoka nje ya eneo la kitongoji cha West Point viungani mwa jiji la Monrovia.Aidha, eneo fulani katika mji mkuu wa Monrovia litatengwa katika harakati za kuthibiti kuenea kwa ugonjwa hatari wa Ebola.
Watu waliojawa na hamaki walishambulia kituo cha afya katika eneo la West Point siku ya Jumamosi, na kupelekea kutoroka kwa wagonjwa 17 wa Ebola.
Hata baada ya Liberia kutangaza hali ya dharura kufuatia mlipuko wa Ebola mapema mwezi huu, ugonjwa huo unazidi kusababisha vifo nchini humo.
Ebola haina tiba lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) liliidhinisha matumizi ya dawa zilizokuwa zikifanyiwa utafiti kufuatia mlipuko mkubwa wa Ebola Afrika Magharibi .
Watu 1,229 wameripotiwa kufarika katika kanda ya Magharibi mwa Afrika tangu ugonjwa huo uzuke miezi minne iliyopita.
Ebola husambazwa moja kwa moja kupitia maji maji ya mwili ya waliougua .
Via: BBC
No comments:
Post a Comment