Tuesday, August 12, 2014

WANAFUNZI WAKALIA MADAWATI KWA ZAMU KUTOKANA NA UPUNGUFU ULIOPO

Hili ni darasa la pili katika shule hiyo  ambapo wanafunzi  zaidi ya 60 darasa moja  hulazimika kukaa kwenye madawati  kwa kupeana  kutokana na upungufu uliopo wa madawati.
  Hii ndio shule ya msingi Kano  katika kijiji cha Amani  huu ni muonekano wake kwa nje.
Huyu ni mwenyekiti wa kijiji cha Amani Dotto Polepole  akielezea changamoto mbalimbali katika shule hiyo na ukosefu wa madawati na kufanya wanafunzi  kuendelea kukaa chini.


Mwalimu mkuu wa shule ya msingi  Kano  Shabani  Masuma alisema katika kero zinazompasua kichwa ni ukosefu wa madawati na maji katika shule hiyo.
  Hiki ni kikao cha serikali ya kijiji cha Amani kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  ambapo  hoja mbalimbali zilikuwa zikielezwa ikiwemo uchangiaji wa madawati kwa kila kaya ili kuweza kupata angalau madawati 30 kwaajili ya wanafunzi wa shule ya msingi  Kano,ambapo mjumbe kwenye kamati hiyo  Zoya Mstapha alisimama na kuchangia hoja kwenye kikao hicho.

WANAFUNZI wanaosoma katika shule ya msingi kano  iliyopo  kijiji cha Amani kata ya Salawe  halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,wanalazimika kusoma kwa kupeana zamu kukaa kwenye madawati kutokana na shule hiyo kukabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati na kusababisha usumbufu wakati wa kuandika.


Akizungumza na waandishi wa habari  waliotembelea kijiji hicho mwalimu mkuu wa shule hiyo Shabani Masuma alisema  wanaupungufu mkubwa wa madawati ambapo yaliyopo ni 50 tu ambapo kuanzia darasa la pili hadi la sita wanakaa chini huku madara mawili la kwanza na la saba ndiyo wamepewa madawati hayo japo kuwa hayatoshi.


Mwalimu Masuma alisema kutokana na changamoto hiyo imekuwa ikisababisha wanafunzi kuwa na muandiko mbaya kwa kuwa hakuna sehemu nzuri ya kukaa ,huku akibainisha kwamba shule hiyo  ina wanafunzi 536 kati yao  wavulana ni 233 na wasichana ni 303  na kwamba darasa moja linawanafunzi zaidi ya 60.


“tunachangamoto ya  uhaba wa madawati yaliyopo ni 50 na wanafunzi  wako zaidi ya 500,wengi wao wanalazimika kukaa chini halafu wachache darasa la kwanza na la saba ndiyo wanakalia madawati ambayo pia hugombania kwa kuwa hayatoshi na kupeana zamu kukaa pia wastani wa wanafunzi 40 hawahudhurii vipindi kutokana na utoro”alisema mwalimu mkuu Masuma.


Mwalimu Magesa  Masolele ni mmoja wa walimu wa shule hiyo alisema  alisema miandiko ya wanafunzi hao inakatisha tamaa hata akiandika  mwanafunzi wa darasa la tano, utafikiri ndio anaanza darasa la kwanza sababu ya kukaa chini hakuna mpangilio mzuri wa mwandiko hivyo inawapa shida walimu hasa katika usaishaji kwenye madaftari  ndio maana  wakaamuwa kupea na zamu kukalia madawati.


Naye  mwenyekiti wa kijiji hicho  Doto Polepole alisema kuwa  changamoto ya uhaba wa madawati ni kubwa kwani hivi sasa serikali ya kijiji imeamua kuanza  kupitisha michango kwa wazazi, ili kuweza kuchongesha madawati wanafunzi wapate unafuu wa kusoma na kuwaondoa kero hiyo.


Baadhi ya wazazi wa kijiji hicho John Mlewa na Samson Masasi walisema kuwa  wazazi wanatoa  michango mingi ya maendeleo na kuweka wazi kuwa suala la madawati halitafanikiwa kwa kupitia wazazi pekee kinachotakiwa ni serikali kuingilia kati suala hilo  ili kuweza kuwakomboa wanafunzi kwani hata wao kama wazazi hawafurahishwi na hatua hiyo.

  wataendelea kukaa chini mpaka lini  hata wao kama wazazi hawafurahii hali hiyo.


Kwa upande wake  kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambaye ni ofisa mipango  Ambokisye Mwakabana alisema kuwa changamoto ya madawati ipo  kwenye shule nyingi na zimetengwa fedha kwaajili ya kuchongesha madawati zaidi ya 500 na kutarajia kusambaza kwenye shule ambazo zinaupungufu  mkubwa kwa kuzipatia madawati 30  kila shule ikiwa kuna shule 128 za msingi katika  kata 26 za wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment