Wanajeshi wawili wa kulinda
amani raia wa Burkina Farso katika shirika la Umoja wa Mataifa wameuawa
na saba wengine kujeruhiwa katika shambulizi la kujitolea muhanga katika
kambi moja ya kupiga doria kazkazini mwa Mali.
Mlipuaji huyo aliendesha gari moja lililojaa vilivupuzi katika kambi hiyo ilio maili 50 kutoka mji wa Timbuktu siku ya jumamosi.David Gressly ambaye ni naibu mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa amesema kuwa wanajeshi wa umoja wa mataifa nchini Mali wanagharamika vilivyo.
Wanajeshi wengine watatu wa kulinda amani pia nao walijeruhiwa katika visa viwii tofauti mapema wiki hii.
Chanzo :bbc swahili.
No comments:
Post a Comment