Monday, August 18, 2014

WIZI WA NYAYA ZA SIMU UNAVYOSABABISHA HASARA KWA SERIKALI


Katibu wa sungusungu Shinyanga John Kadama akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika shule ya msingi Bugoyi kata ya Ndembezi kwa lengo la kujadili kuibuka kwa wizi wa nyaya za simu za kampuni ya TTCL pamoja na uharibifu wa miundombinu ya barabara ,reli na nyaya za umeme.
Naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara ambapo alisema kukithiri kwa wizi wa nyaya za simu kuna tokana na vijana kujiingiza katika makundi maovu ikiwa ni pamoja na kuvuta bangi na madawa ya kulevya na kuiomba jamii kuwafichua wanaofanya uhalifu. Kwa mujbu wa TTCL tangu mwaka huu uanze tayari wamepata hasara zaidi ya milion 133 kutokana na wizi wa  nyaya za simu.
Baadhi ya viongozi wa serikali wakiwa kwenye mkutano huo
Mkutano unaendelea wananchi wakifuatilia kwa makini na kuchukuwa mambo muhimu.
Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede akiwataka wananchi kutoa taarifa za wahalifu kwa kuwa miongoni mwao wanawafahamu wanaofanya wizi huo na kusababisha upotevu wa mamilion ya fedha za serikali.
Viongozi kutoka jeshi la polisi wakifuatilia kilichokuwa kinajadiliwa juu ya kukomesha wizi wa nyaya za simu za TTCL sanjari na kukomesha vitendo vya uhalifu.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.


                       
        






No comments:

Post a Comment