Aliyewahi kugombea ubunge wa Mlalo Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwaka 2005, Charles Kagonji amekihama chama hicho na kurejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kagonji
alirejea CCM katika mkutano wa hadhara, uliofanyika Sunga Kata ya Sunga
Tarafa ya Mtae wilayani Lushoto, jana, mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana.
Kagonji amekaa katika chama hicho kikubwa cha upinzani kwa miaka minne, kabla ya kuamua kukihama jana.
Kabla
ya kujiunga na Chadema, Kagonji ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa
Habari, aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Mlalo kwa miaka 15 kutoka
mwaka 1990 hadi mwaka 2005 kwa tiketi ya CCM.
Kabla
ya kuwa mbunge, Kagonji ambaye alikuwa mpigapicha maarufu na mwandishi
wa habari mwandamizi, alifanya kazi kwa miaka mingi katika Idara ya
Habari (Maelezo).
Akihojiwa
kwa njia ya simu jana sababu zilizomfanya ahame Chadema, alisema kuwa
ameamua kurudi nyumbani (CCM), kwa sababu ndiyo iliyomlea na anafahamu
vizuri historia, mila na desturi zake.
Alisema
Chadema hajui mila na desturi zake, lakini ni chama kizuri na chenye
nguvu, bali yeye ameamua kurejea nyumbani. Kagonji alisema alipokuwa
Mbunge wa Mlalo, alijitahidi kufanya mambo mengi makubwa ya maendeleo
kwa kushirikiana na wananchi.
Kwa
mfano, alisema akishirikiana na wananchi, walijitahidi kuanzisha shule
za sekondari za kata na hadi anaondoka mwaka 2010, jimbo hilo lilikuwa
na sekondari 10. Kwa sasa sekondari zimeongezeka hadi zaidi ya 16.
No comments:
Post a Comment