Meli ya Mv Victoria inayo fanya safari
zake kati ya mikoa ya Mwanza na Kagera katika ziwa Victoria imenusurika
kuzama karibu na bandari ya kemondo nje kidogo ya mji wa Bukoba tukio
ambalo limesababisha meli hiyo kushindwa kuendelea na safari yake.
Wakiongea baada ya abiria waliokuwa wanasafiri na meli hiyo
kutoka mjini Bukoba kwenda mwanza wamesema meli hiyo imekuwa ikipata
hitilafu za mara kwa mara bila kuchukuliwa hatua na kwamba katika safari
ya jana meli hiyo iliondoka mjini Bukoba saa tatu usiku lakini ilizima
mara tatu ndani ya maji na hivyo ikachelewesha safari ya meli hiyo
ambayo ilifika katika bandari ya Kemondo saa tisa usiku na kuleta
usumbufu na wasiwasi kwa abiria waliokuwa wanasafiri na meli hiyo.
Kwa upande wake nahodha wa meli hiyo John Mwita amesema meli hiyo
ilipata hitilafu kutokana na usukani kuwa mbovu hali ambayo
ilisababisha meli hiyo kuzimika mara kwa mara na kwamba tayari kampuni
ya huduma za meli imeagiza vipuri kwaajili ya matengenezo ya meli hiyo
ambayo inatarajiwa kuendelea na safari baada ya matengenezo kukamilika
ambapo meneja wa bandari ya Kemondo Joashi miso amesema meli hiyo
ilikuwa na abiria zaidi ya mia nne na hamsini na tani mia moja na
hamsini za mizigo na amewataka abiria kuwa watulivu wakati taratibu za
kutatua tatizo hilo zikiendelea.
No comments:
Post a Comment