Sunday, October 12, 2014

HAYA NDIYO YALIYOJIRI SHINYANGA KUPITIA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA,PATA TUKIO ZIMA HAPA.

Meneja wa shirika la nyumba mkoa wa Shinyanga Ramadhan Macha akisoma taarifa kwenye hafla fupi ya kukabidhi mashine 20 za kufyatulia matofali kwenye ukumbi wa jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa ambazo zimetolewa na NHC ili kutoa ajira kwa vijana katika halmashauri za mkoa huo,ambapo kila kikundi cha vijana 40 watapatiwa mashine moja itakayotumika katika hughuli za kufyatua matofali na kusaidia kuongeza kipato chao sanjari na kuondoa umasikini nchini.
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselm Tarimo akikabidhi mashine kwa viongozi kutoka kila halmashauri,huku akisisitiza kuhakikisha wanazitunza ili ziwe na tija kwa vijana.
Mtaalamu wamshine za kufyatua matofali kutoka chuo cha maendeleo ya wananchi wilayani Kahama (MWAMVA) Augustino Maige akitoa maelezo kwa katibu tawala mkoa wa  Shinyanga Anselm Tarimo jinsi mashine zinavyofanya kazi.
Baadhi ya wafanyakazi wa NHC wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katibu tawala wa mkoa huo Tarimo aliyevaasuti,wa kwanza kushoto ni meneja wa NHC Ramadhan Macha na wa kwanza kulia baada ya mgeni rasmi ni mhasibu mkuu wa mkoa NHC Frenk Magili.
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselm Tarimo akizungumza  na watumishi wa NHC pamoja na viongozi wa halmashauri kabla ya kukabidhi mashine hizo,ambapo alitahadharisha kuwa vikundi vya vijana visitumiwe kama vijiwe vyasiasa au  magenge ya kuficha wahalifu na kuwaasa maafisa vijana wa kila wilaya kuhakikisha wanasimamia kikamilifu na kutoa taarifa.
Wakifuatilia maelekezo ya katibu  tawala mkoa.
Viongozi kutoka halmashauri za mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa NHC  mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi mashine.
Picha za  kumbkumbu zinaendelea kutoka kwa viongozi mbalimbali.



                                   











No comments:

Post a Comment