Mashabiki wa Yanga wakifurahia ushindi ni baada ya kuinyuka timu ya Stend United goli 3-0 katika mechi iliyopigwa jana uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga huku maelfu ya mashabiki wa timu hizo wakifulika uwanjani kushuhudia.
Wakati timu ya Simba ikiendelea kutofanya vizuri katika mechi zake baada ya kulazimishwa tena
sare ya bao moja kwa moja na maafande wa Prisons katika Uwanja wa
kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, wakati mahasimu wao Yanga wakipata
ushindi mnnono wa 3-0 dhidi ya Stand United mjini Shinyanga.
Yanga imefikisha pointi kumi baada ya kucheza michezo mitano na
kuwacha mahasimu wao Simba nyuma kwa pointi tano baada ya kupata sare
yake ya tano kutokana na michezo yake mitano.
Tofauti na furaha na nderemo za Wanajangwani, Simba mambo si shwari,
kwani matokeo haya mabaya sana tangu kuanzishwa kwake kwa kuambulia
pointi tano kutokana na mechi tano ambayo yanaifanya timu hiyo kupoteza
jumla ya pointi kumi tangu kuanza kwa msimu huu wa Vodacom Premier
League.
Ilionekana kama Simba ingepata ushindi wake wa kwanza jijini Mbeya
baada ya kuongoza kwa kipindi kirefu, lakini ndoto yao ilikatishwa
katika dakika za majeruhi baada ya Prisons kusawazisha.
Simba ilipata bao la kuongoza kupitia kwa Mganda Emanuel Okwi kabla
ya Prisons kuchomoa dakkika za majeruhi kupitia kwa Hamisi Mahingo.
Tofauti na matokeo ya Mbeya, Yanga imeweza kupata ushindi wake wa kwanza mnono.
Mbrazil Geilson Jaja alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 13 kwa bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza kisha mabao mengine mawili kufungwa na Tegete.
Pichani ni wachezaji wa Stend United wakiwa tayari kuingia uwanjani kupambana na yanga hata hivyo waliambulia kichapo cha goli 3-0 . |
No comments:
Post a Comment