KITU ambacho kinadhaniwa kuwa ni bomu kimelipuka ndani ya gari na kuuwa mtu mmoja na kuwajeruhi watatu jana tarehe
01/11/2014 muda wa saa 07:45hrs katika center ya Mhunze tarafa ya
Kishapu na Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Gari
hilo lenye namba za usajili T. 848 AKA MITSHUBISH FUSSO
likiendeshwa na Khalifa s/o Mussa 39, muhangaza wa Ngara ambalo lilitoka
tarehe 31/10/14 saa 04:00 hrs mjini Ngara kuja Mkoa wa Shinyanga wilaya
ya Kishapu kupakia shehena ya mtama kwa mfanyabiashara alitwaye Donard
s/o Nzugula (49) mkazi wa Muhunze.
Inaelezwa
kuwa wakati gari hilo likiwa limeegeshwa dukani kwa mfanyabiashara huyo
ili kusubiri kupakia mzigo huo dereva alishuka kununua sigara maduka ya
jirani akamwacha utingo wake ndani ya gari peke yake ambaye anaitwa
Juma s/o Rashid 21-23, mkazi wa Ngara ambaye ni familia ya mwenye
gari(aliyefariki dunia)
Baada
ya muda mfupi kama dakika 15 hivi dereva alisikia mshindo mkubwa na
alipokwenda kwenye gari alimkuta utingo wake ametupwa nje ya gari na
akiwa amefariki mwili wake ukiwa na majeraha tumboni,mkono wa kushoto
kiganja kimekatika,mkuu wa kulia kwenye paja ambalo limechimbika hadi
kwenye mfupa, shingoni upande wa kushoto kuna shimo kubwa
lililosababishwa na kitu chenye ncha kali.
Pia
mfanyabiashara Donard Nzugirwa Mwalimu ambaye ameumia mkono wa kulia
kwa kuchanwa chanwa na vipande vya chuma,amepelekwa hospitali ya mkoa
kwa matibabu zaidi.
Wengine ni Maganga Pius (14 ), mkazi wa Kishapu ambaye amejeruhiwa paja la kushoto,mgongoni na mkono wa kushoto.
Seni Edward (25 ), ambaye amejeruhiwa bega la kushoto, majeruhi wote wametibiwa na kuruhusiwa. Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

No comments:
Post a Comment