Tuesday, November 25, 2014

WAASWA KUTOKIMBILIA KWA WAGANGA WA KIENYEJI KUPATIWA MATIBABU

Wananchi wa kata ya Nyalikungu wilayani Maswa mkoa wa Simiyu wameaswa kuacha tabia ya kwenda kutibiwa kwa waganga wa kienyeji badala yake waende kwenye vituo
vya afya vilivyopo kwenye maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kujiunga na mfuko wa bima ya afya CHF kwa kutoa sh 10,000 kwa kaya na kutibiwa bure watu sita mwaka mzima.  Rai hiyo aliitoa jana mkuu wa wilaya hiyo Luteni mstaafu Abdalah Kihato wakati akizindua kwa mara nyingine huduma za CHF,alisema inasikitisha kuwepo  mwitikio mdogo wa wananchi kujiunga na mfuko huo badala yake wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji na kutoa gharama kubwa huku wengine wakitakiwa kupeleka mbuzi na kuwataka gharama hizo kuwekeza kwenye afya kwani wakiugua wakiwa hawana kadi za CHF watatibiwa kwa gharama kubwa.


Wananchi wakifuatilia kwa makini nasaha zilizokuwa zikitolewa na wataalamu mbalimbali kwenye uzinduzi wa mfuko huo katika viwanja vya nguzo nane mjini Maswa  ambao wanawake wengi ndiyo waliojitokeza huku idadi ya wanaume ikiwa ndogo.

Mkuu wa  wilaya ya Maswa Abdalah Kihato  akisisitiza  umuhimu wa kujiunga na CHF kwani mfuko  huo upo kwa ajili ya wananchi ambao watakaokuwa wanachama watapata matibabu ndani ya wilaya kupitia vituo vyote vyaserikali  zahanati,vituo vya afya na hospitali nakuwapunguzia mzigo wa kuanza kutafuta fedha za matibabu pindi watakapougua ghafula.

Meneja wa mfuko wa bima ya afya mkoa wa Shinyanga Emmanuel  Amani,akiwataka wananchi kuacha kuona ufahali wanapokuwa na mali nyingi ama mifugo na kuwashauri kuwekeza zaidi kwenye matibabu,pindi watakapougua  waweze kutibiwa bure watu sita katika kaya mwaka mzima kwa kulipia sh 10,000 tu.                                                                                                                               Alisema  mfuko huo wa CHF utakuwa na faida kwa wananchi iwapo watajiunga  wengi ili fedha zitakazopatikana  zitatumika kununua dawa huku akitoa mfano kuwa wao wakichangia milion moja serikali nayo itaongeza milioni moja na kufika mbili ambapo zote zitatumika kununua dawa na vifaa tiba  huku akitahadharisha  kuwa utaratibu wa CHF hauondoi utaratibu wa serikali  wa kupeleka dawa kwenye vituo.
Uzinduzi  wa CHF kwa mara nyingine unaendelea
Afisa matekelezo na uratibu kutoka makao makuu ya mfuko wa bima ya afya NHIF jijini Dar  es salaam Catherine Masingisa  akiwataka wananchi kuhakikisha wanasimamia mapato na matumizi kutokana na michango yao waliyoitoa,kwa kuzishinikiza kamati za afya za vituo walizochagua ili kuhakikisha  dawa zinakuwepo za kutosha na vifaa tiba.
Mganga mkuu wa wilaya ya Maswa akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo ambapo aliweka wazi kuwa hakuna idadi ya magonjwa yatakayotibiwa  kupitia mfuko wa CHF  isipokuwa watakaokwenda kutibiwa nje ya wilaya hiyo.
Vijana wakionyesha igizo ambalo lilikuwa likielimisha jamii umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.
Katibu wa afya wilaya ya Maswa
Masige Jumanne akitoa  taarifa ya mfuko wa CHF,alisema hali ni mbaya kutokana na idadi ya wachangiaji  kuzidi kushuka na wengine kwenda kwa waganga wa kienyeji,ukosefu wa   dawa za kutosha kwenye  vituo pamoja na uhaba wa wataalamu wenye sifa ni mambo yanayo kwamisha mfuko  huo ambapo  aliwataka wananchi kujiunga kwa wingi ili dawa zinunuliwe za kutosha.







No comments:

Post a Comment